WEWE MWENYEWE UTAZIONGEZA GHARAMA ZA UJENZI UNAZOJITAHIDI SANA ZIPUNGUE.
Kwa kawaida watu wengi sana hupenda hadithi ya kupunguza gharama za ujenzi na hilo huwa ni kipaumbele cha wengi kuliko kipengele kingine cha ujenzi. Lakini watu hufikiria sana kuhusu kupunguza gharama za ujenzi wakiwa bado hawajui gharama hizo zinahusu nini haswa na zina umuhimu gani zinapokuwa katika kiwango hicho. Watu hubaki kuogopa na kutaka sana kupunguza gharama wakiwa hawajui haswa kwa nini zimekuwa hizo ila huongozwa na hisia kukimbilia kupunguza ili wajisikie vizuri na urahisi wa kihisia kwamba wamepungu za gharama kabla ya kujua undani wake.
Lakini pale ambapo mtu anaingia kwenye mchakato na kukutana na mambo mengi na kuhitajika kufanya machaguo baada ya kujua undani wa gharama husika za ujenzi, pamoja na faida zake na changamoto zake ndipo utakuta mtu anaridhia kufanya machaguo ambayo wakati mwingine ni ya gharama kubwa zaidi na kuongeza gharama za ujenzi kwa sababu anakuwa ameshajua haswa kile anachohitaji.
Jambo hili hutokea kwa karibu kila mtu ambapo kutokana na ule umhimu wa machaguo husika ambao unazidi umuhimu wa ukubwa wa bei ambao kwa wakati huo huonekana kuwa si kitu. Hivyo mtu unapokuwa unapanga kuhusu ujenzi na kuweka bajeti kiasi ambacho umepanga utahakikisha bajeti hiyo inakamilisha ujenzi ni vyema kuweka dharura kwa sababu ni hakika kwamba wakati wa kufanya machaguo ya huduma na bidhaa, hususan bidhaa utajikuta unalazimika kuongeza kutokana na umuhimu wa kile ambacho umeshakifahamu kiundani.
Karibu sana.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!