KUHIFADHI MAJENGO YA KALE AU KUJA NA UBUNIFU WA KISASA.

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

Ellsworth Toohey ni mwandishi mwenye fikra za kijamaa. Ellsworth Toohey anaandika kuhusu makala mbalimbali za kwenye magazeti na anaandika sasa kuhusiana na taaluma ya Usanifu Majengo.

– Kwanza Ellsworth Toohey anaandika kuhusu historia ya Usanifu Majengo kuanzia nyakati za Misri ya kale, Ugiriki ya kale, Rumi ya kale na nyakati zilizofuata. Anajaribu kuonyesha namna taaluma ya Usanifu Majengo ilikuwa na mchango kwa watu wa kawaida katika nyakati mbalimbali katika historia.

– Ellsworth Toohey anajaribu kuonyesha kwamba falsafa ya taaluma ya Usanifu Majengo hasa katika Majengo ya umma inatakiwa itokana na wananchi wa jamii husika. Anajaribu kupingana na ushujaa wa mtu mmoja na uwezo mkubwa na vipaji vya mtu binafsi katika kufanya kazi yenye ubora na badala anashinikiza kwamba jengo linapaswa kutokana na mawazo ya wengi na liwe limefanywa na umma.

– Henry Cameron anazidi kuwa katika wakati mgumu zaidi kwa ofisi yake kukosa kazi kiasi cha kushindwa hata kulipia baadhi ya huduma muhimu. – Mwezi February mwaka 1925 Henry Cameron anastaafu kazi yake ya Usanifu Majengo na kufunga ofisi yake. Henry Cameron anastaafu baada ya kuumwa na kupelekwa hospital kisha daktari kumwambia kwamba ikiwa ataondoka kitandani na kwenda kufanya kazi atakuwa amejipa mwenyewe hukumu ya kifo.

– Mrs. Keating mama yake na Peter Keating anapangisha nyumba yake ya Stanton na kisha kuondoka kuelekea New York kwenda kuishi na mtoto wake Peter Keating.

– Peter hafurahii sana kuishi na mama yake lakini hawezi kukataa kwa sababu ni mama yake.

– Mrs. Keating, mama yake na Peter anakuwa karibu sana na Peter anajaribu kutembelea mpaka ofisi kwao na kumweleza ni namna gani anatakiwa kuwa bora kuzidi wote ofisini kwao. Anaonekana kutofurahia pale anapogundua kuna mfanyakazi yeyote anayemzidi Peter kwa jambo lolote kwa sababu anamuona kama mshindani na kikwazo kwa Peter.

– Mama yake Peter anamfahamu Catherine alimwona huko Stanton mara kadhaa lakini hampendi wala kumkubali, anafikiri kwamba Peter anatakiwa kupata mwanamke bora zaidi.

– Anajaribu kumuuliza Peter kama anafahamiana na watoto wa Guy Francon na anaonekana kutamani Peter ajaribu kuimarisha mahusiano na binti wa Guy Francon.

– Baadaye Peter anamuuliza Guy Francon kuhusiana na binti yake na Guy Francon anamwambia kwamba binti yake ni mwandishi wa makala. Lakini hafikiri kwamba Peter atavutiwa naye. Guy Francon anasema kwamba yeye mwenyewe havutiwi na namna binti yake amekuwa. Anasema kwamba anahisi alifeli kwenye malezi.

– Howard Roark anachoma moto baadhi ya nyaraka Henry Cameron kama alivyoagizwa na Henry Cameron mwenyewe na kufunga ofisi hiyo.

– Peter Keating anamtembelea Howard Roark nyumbani kwake na kumtaka wakafanye kazi pamoja kwenye ofisi ya Francon & Heyer. Howard Roark anakubali na kukubali pia mshahara wa kulipwa dola 65 kwa wiki.

– Howard Roark anaweka masharti na kwenda kufanya kazi kwenye ofisi hiyo lakini akiwa ameletwa na Peter huku Guy Francon akiwa hana ukaribu naye wala kujishughulisha naye.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *