USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 23 KURITHI KAMPUNI YA UJENZI

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Ellsworth Toohey anaonekana kubadili msimamo wake kuanza kuunga mkono mitindo ya kisasa ya Usanifu Majengo. Anajaribu kuonyesha kutambua mchango wa Henry Cameron katika harakati za kupigania mitindo ya kisasa ya Usanifu Majengo.

2. Guy Francon anatangaza kustaafu na kumwachia Peter Keating kampuni ya Francon & Keating. Peter Keating anakuwa ndiye mmiliki na mkurugenzi pekee. Peter Keating anamwambia Guy Francon kwamba yeye na Dominique wameachana na Guy Francon anamwambia hawezi kumlaumu juu ya hilo pengine sio kosa lake wala la Dominique.

3. Peter Keating anaanza mradi wa Stoneridge katika hatua ya michoro. Anawaagiza wafanyakazi wake Neil Dumont na Bennet wafanye kazi yoyote nzuri, vyovyote vile lakini iwe nzuri.

4. Peter Keating anaona majukumu ya kuiendesha kampuni peke yake ni mazito sana hivyo anatafuta mshirika. Anaamua kumchukua Neil Dumont kama mshirika wake.

5. Wanabadilisha jina la kampuni kutoka kuitwa Francon & Keating na kuanza kuitwa rasmi Peter Keating & Cornelius Dumont. Wanafanya sherehe ndogo ambayo hata hivyo Peter Keating anashindwa kuhudhuria kwa sababu alisahau.

6. Mradi wa Stoneridge ndio mradi wa mwisho ambao umefanywa na kampuni ikiwa kama Francon & Keating. Cornelius Dumont sio mtu mwenye hamasa sana na kazi wala kampuni, yuko zaidi kama Lucius Heyer.

7. Dominique anafika New York akitokea Ohio na moja kwa moja anakutana na Gail Wynand akimsubiri.

8. Gail Wynand anamchukua Dominique kwenye gari yake na kuondoka. Dominique japo yuko kimya lakini hajui wanapoelekea. Anamuuliza Gail Wynand.

9. Gail Wynand anamjibu kwamba wanaenda kwa mwanasheria kufunga ndoa. Dominique anamwambia Wynand yeye angependelea ndoa itakayofungwa hadharani kila mtu aone, iwe na sherehe kubwa na waalikwe watu mashuhuri.

10. Gail Wynand anamwambia hiyo inahitaji angalau wiki moja ya maandilizi ili angalau kuwaandaa watu na sherehe hiyo. Kisha anaanza kuishughulikia.

11. Harusi ya Dominique na Gail Wynand inafanyika. Watu wengi mashuhuri wanahudhuria akiwemo Guy Francon baba yake Dominique. Guy Francon anasema ni vizuri na anashukuru sana ikiwa Dominique ana furaha kwani kitu muhimu kwake ni kumuona Dominique akiwa mwenye furaha.

12. Watu wengine mashuhuri wakiwemo wafanyakazi wa “The New York Banner” wanahudhuria akiwemo Ellsworth Toohey na Alvah Scarret lakini hawaruhusiwi kupiga picha wala kuripoti matukio zaidi ya kile kidogo kilichoamuliwa na Guy Francon.

13. Sherehe inakwisha na maisha ya ndoa kati ya Dominique na Gail Wynand yanaanza rasmi.

14. Sally Brent akiwa kama mfanyakazi mzoefu wa “The New York Banner” anaamua kuandika kuhusu maisha ya faragha ya mapenzi kuhusu Dominique na Gail Wynand. Taarifa zinamfikia Gail Wynand ambaye anamfukuza kazi Sally Brent.

15. Alvah Scarret anajaribu kumtetea Sally Brent kwa Gail Wynand na kumwambia hawezi kumfukuza Sally Brent kutokana na umuhimu mkubwa kwenye “The New York Banner” na idadi ya wasomaji wanaomfuata ambao watawapoteza kwa kumfukuza kwake.

16. Gail Wynand anamwambia siku ambayo atashindwa kumfukuza mfanyakazi ni siku ambayo atafunga ofisi hizo na kulipua jengo zima kuliteketekeza.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *