USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 22 DOMINIQUE NA GAIL WYNAND
KITABU: FOUNTAINHEAD.
AUTHOR: AYN RAND.
1. Dominique na Gail Wynand wanaondoka na boti ya kifahari ya Gail Wynand inayoitwa “I DO” na kwenda safari ya siku kumi mapumzikoni. Wanazungumza kuhusiana na topiki mbalimbali za falsafa kwa muda mrefu sana.
2. Gail Wynand anavutiwa sana na Dominique na kumshawishi waoane. Anasema haitoshi kuwa hawara peke yake bali wanahitaji kuoana kabisa.
3. Dominique anamwambia kama hicho ndicho atakachokitaka ni sawa wataoana lakini anafikiri wataoana kwa siri. Gail Wynand anamwambia hapana anataka waoane kwa uwazi.
4. Anarudi na Gail Wynand anampa Peter Keating mkataba wote wa kujenga jengo la Stoneridge. Kisha anamwambia kwamba anahitaji kumuoa Dominique.
5. Ellsworth Toohey anapata habari kutoka kwa Peter Keating kwamba Gail Wynand anamuoa Dominique. Ellsworth Toohey anashtuka na hafurahii habari hizo. Anafikiria kwa haraka nini cha kufanya.
6. Ellsworth Toohey anamtafuta Alvah Scarret kumshawishi wajaribu kuzuia ndoa ya Dominique na Gail Wynand. Alvah Scarret anashawishika na kuona kwamba kweli haitaleta picha nzuri kwenye jamii kwa bosi wao huyo kumuoa mwanamke kama Dominique kwa namna anavyojulikana.
7. Alvah Scarret anaonana na bosi wake Gail Wynand na kujaribu kumshawishi aachane na mpango wa kumuoa Dominique. Gail Wynand anamwambia aachane kabisa suala hilo, na mjadala huo.
8. Gail Wynand anamwagiza Alvah Scarret kuweka tangazo la ndoa yao kwenye gazeti ya “The New York Banner”.
9. Dominique baada ya kurudi New York anakwenda kumuona Steven Mallory kumuuliza alipo Howard Roark. Steven Mallory anamjibu kwamba Howard Roark hayupo New York, bali alikwenda Ohio ambapo kuna kazi anafanya huko.
10. Dominique anaelekea Ohio kumfuata Howard Roark kujua anaendeleaje. Dominique anafika Ohio na kufanikiwa kumpata Howard Roark ambapo wanaongea kwa kirefu sana.
11. Dominique anamwambia Howard Roark kwamba anaolewa tena kwa mara nyingine. Lakini safari hii anaolewa na Gail Wynand na sio Peter Keating tena. Anamuuliza Howard Roark ni yupi afadhali kati yao na anamjibu kwamba ni afadhali tena Peter Keating.
12. Howard Roark anakumbuka maneno ya Henry Cameron juu ya Gail Wynand kwamba ndio anayetakiwa kuwa naye makini zaidi na kupambana naye sana. Ni mtu hatari sana.
13. Dominique anamwambia Howard Roark kwamba anahitaji kuhamia pale Ohio alipo amsaidia kufanya kila kitu anachohitaji. Anamwambia atahamia kama alivyo na wala hatachukua pesa yake yoyote, ataishi naye kama alivyo. Howard Roark anamwambia aachane na mpango na aendelee na mpango wake wa kuolewa na Gail Wynand.
14. Howard Roark anamsindikiza Dominique kituoni kwenda kupanda treni kurudi New York. Dominique anaonekana kuifurahia sana Ohio kwa sababu Howard Roark yupo huko na kujaribu kutunza kumbukumbu zake za Ohio.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!