USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 25 URAFIKI WA MAWAZO

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Gail Wynand anamjulisha Dominique kwamba Howard Roark aliyejenga Stoddard Temple na kupata ukosoaji mkubwa atakuja kupata chakula cha jioni na wao hapo nyumbani na ndiye aliyemchagua kujenga nyumba yao mpya nje ya mji.

2. Dominique anamuuliza Gail Wynand kwa nini ameamua kumchagua Howard Roark kujenga nyumba yao. Anamjibu kwamba karibu kila jengo zuri lililomvutia alilokutana nalo mjini alipoulizwa aliyelijenga aliambiwa ni Howard Roark ndio maana akamtafuta.

3. Howard Roark anafika nyumbani kwa Gail Wynand kupata chakula cha jioni kama alivyoalikwa na anamsalimia Dominique kwa jina la Mrs. Wynand.

4. Howard Roark anamwambia Dominique kama amependa michoro ya majengo ya nyumba yao ni kwa sababu ya mawazo bora ya Gail Wynand yaliyowasilishwa kwake na Gail Wynand tangu mwanzoni.

5. Siku inayofuata Gail Wynand anatoka ofisini kwake jioni na kwenda ofisini kwa Howard Roark ambapo wanaongea kwa kirefu sana hususan kuhusiana na falsafa na mambo mengine na taratibu wanaanza kuwa marafiki. Gail Wynand anapata amani sana kuwepo ofisini kwa Howard Roark.

6. Gail Wynand anakutana na Ellsworth Toohey na kumwagiza asitishe kuandika habari zozote kuhusiana na Howard Roark tangu sasa kwenye gazeti la “The Banner”. Ellsworth Toohey anamjibu kwa kipindi hiki hataandika kuhusu Howard Roark.

7. Gail Wynand wanakutana tena na Howard Roark kupata chakula cha mchana, wanazungumza sana na kufurahi pamoja. Gail Wynand anamuuliza Howard Roark kama amewahi kupenda mwanamke, Roark anamjibu hata sasa bado yuko kwenye hali ya kumpenda mwanamke. Gail Wynand anamwambia lakini kufanya ujenzi anapata starehe kubwa kuliko kuwa katika mapenzi na mwanamke. Howard Roark anamjibu ni kweli yeye kujenga kwake ni starehe kubwa zaidi kuliko kuwa katika mapenzi na mwanamke.

8. Ellsworth Toohey, Mitchell Layton, Homer Slottern, Jessica Pratt, Eve Layton, Lois Cook, Jules Fougler, Lancelot Clokey, Gordon Prescott na Renee Slottern wanajadili mada za falsafa mbalimbali na kuwakosoa watu wanaishi falsafa tofauti kama vile Gail Wynand.

9. Peter Keating amepoteza umaarufu na nafasi ya kupata kazi mbalimbali kwa sababu Ellsworth Toohey ameacha kumwandika na kumsifia kama Msanifu Majengo mkubwa kama zamani.

10. Peter Keating anamwita mama yake waje waishi naye tena pamoja wakati huu Peter Keating ana miaka 39.

11. Mama yake anamshauri Peter Keating kuoa na anampendekeza kwake Catherine Halsey. Peter Keating anamsikiliza lakini hamjibu chochote.

12. Kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa makazi ya watu wengi unakuja unazungumziwa unaoitwa Cordlandt ambao Peter Keating anatamani sana kuupata lakini amekata tamaa kabisa kwamba ataweza kuupata kwa sasa.

13. Neil Dumont anamwambia aongee na rafiki yake Ellsworth Toohey kwani ndiye mtu mwenye ushawishi zaidi anayeweza kumpigania akapata mradi huo. Peter Keating anasita lakini baadaye anasema atazungumza naye wala haogopi.

14. Peter Keating anaenda ofisini kwa Ellsworth Toohey na kujaribu kumshawishi ampiganie kupata mradi wa Cordlandt. Ellsworth Toohey anamwambia Peter Keating mpaka leo bado hajamwelewa, bado hajaelewa falsafa zake wala misimamo yake.

15. Peter Keating na Ellsworth Toohey wanaongea sana na mwisho Ellsworth Toohey anamwambia Peter Keating kama ataweza kutimiza vigezo vya kupata mradi huo atajitahidi kumpigania.

16. Mradi wa Cordlandt ni mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya watu wa kipato cha chini, ni mradi mkubwa na Ellsworth Toohey anampatia Peter Keating maelezo yote na nyaraka akazifanyie kazi.

17. Peter Keating anakwenda ofisini kwake na kukaa akifikiri sana namna ataweza kufanikisha kufikia vigezo vya mradi huo hasa kuhusiana na gharama. Baada ya kufikiri sana kwa siku kadhaa anapata wazo la kwenda kwa Howard Roark kupata mawazo yake au suluhisho japo anasita kwa sababu ya ile kesi ya Stoddard Temple na ule mradi mwingine.

18. Wakiwa hawajawahi kuonana kwa kipindi cha takriban miaka sita Peter Keating anafika ofisini kwa Howard Roark na kusalimiana naye.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *