CHANGAMOTO ZISIZOTARAJIWA KWENYE UJENZI.

Moja kati ya changamoto kubwa ambayo mara nyingi huwa tunakutana nayo kwenye ujenzi ni kukutana na changamoto usiyoitarajia. Changamoto zisizotarajiwa hutokea wakati wowote na kuleta usumbufu mkubwa na wakati mwingine hata hasara kwa sababu inaweza kuwa ni changamoto ambayo utatuzi wake unakuwa sio rahisi. Changamoto hizi tunapokutana nazo zinayumbisha sana mradi wa ujenzi kwa sababu zingeweza kufahamika mapema zingetatuliwa kwa urahisi lakini kuchelewa kwake kumekuwa ni changamoto kubwa.

Leo nataka nizungumzie moja kati ya changamoto isiyotarajiwa kwenye ujenzi na imekuwa ni moja ya matatizo makubwa katika mradi wa ujenzi. Changamoto hii ni vifaa vilitumika kwenye jengo kumalizika kwenye ghala na kutopatikana tena wakati ndio zinategemea katika kuhakikisha jengo linakuwa na ufanano mfululizo. Mara nyingi tunapokwenda kuchukua mzigo wa vifaa vya ujenzi kama vile vigae vya sakafuni huwa tunachukua idadi ambayo tunatazamia kuitumia ujenzi utakapoanza au wakati unaendelea. Baadaye baada ya kutumika kisha havikutosha na hivyo ikawalazimu watu kurudi kwenye ghala kwa ajili ya kuongeza idadi mara nyingine hukuta vimemalizika na havipatikani tena vya namna hiyo.

Unapokuta vifaa hivyo vimemaliza yaani viko nje ya stock na kiwanda kinachukua muda mrefu sana kuzalisha au mara nyingi hakizalishwi tena basi mahali vilipotumika kunakosena vifaa sahihi vya kuweka hapo kitu ambacho kinapelekea muonekano na ule umaridadi kupotea na hivyo kupunguza hadhi ya jengo. Changamoto hii imekuwa ikitokea bila kutarajiwa na wadau wengi wa ujenzi ikiwemo wateja ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu sana wa namna ya kuitatua. Jambo muhimu la kuzingatia hapa ni muhimu kwamba pale mtu unapoamua kuchukua vifaa fulani vya ujenzi ambavyo unajua kwamba stoku yake huisha kwenye stoo ilipo na haitafaa kuja kuchanganya na aina nyingine ya hivyo kwenye vifaa ni muhimu sana basi mtu ukahakikisha unachukua kiasi cha kutosha wakati unanunua pamoja na akiba kidogo ili kuepuka kukutana na changamoto kama hiyo.

Kwa mfano ikiwa unanunua vigae fulani vya aina fulani labda kutoka Ujerumani, Uhispania au Italia na kwamba vinaenda kutumika eneo fulani muhimu na lenye muonekano maridhawa kiasi kwamba haitafaa kuja kuchanganya na aina nyingine ni muhimu sana kuhakikisha idadi uliyochukua inatosha kumaliza sehemu ya mradi husika wa ujenzi. Vinginevyo basi ujiandae kuja kuchanganya na aina nyingine isiyoendana na inayoonyesha kwamba kuna tatizo katika mpangilio huo na hasa kupunguza hadhi ya jengo hilo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *