MIKOPO MINGI YA UJENZI(MORTGAGE) HAITOLEWI FEDHA TASLIMU WALA FEDHA YOTE.
Mikopo ya ujenzi inayojulikana zaidi kitaalamu kama “mortgage” ambayo hutolewa kwa namna tofauti na mikopo ya biashara ni mikopo ambayo bado haina miaka mingi sana kwa nchi nyingi zinazoendelea. Mikopo hii pia inapewa muda mrefu sana wa kurudisha ambapo inafika mpaka miaka 20 ya marejesho mpaka kumaliza mkopo wenyewe. Lakini kwa kuwa lengo lake ni kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi kukamilika basi fedha hiyo ni mara chache sana kutolewa kama fedha taslimu bali inalipwa moja kwa moja kwa watoa huduma na bidhaa zinakwenda kukamilisha ujenzi husika.
Hili linafanyika hivi ili kusaidia kudhibiti tamaa za watu ambao huchukua mkopo kwa ajili ya lengo lingine na kwenda kufanyia jambo jingine kitu ambacho husababishia taasisi hizi za kifedha kupata shida sana katika kutimiza malengo yake na hususan kupata marejesho yaliyokubaliana na kwa wakati. Lakini pamoja na hayo bado taasisi hizi za kifedha kwa sehemu kubwa huwa hawatoi mkopo wote kwa ajili ya ujenzi bali baadhi ya taasisi au benki hutoa sehemu kubwa ya mkopo na sehemu iliyobaki huhitaji mteja mwenyewe kumalizia kiasi hicho cha fedha.
Benki inaweza kwa mfano kutoa asilimia 80% ya gharama zote au fedha zote kisha kumtaka mteja kumalizia asilimia 20% baada ya kuwa amekamilisha vigezo na masharti mengine waliyompa. Lakini taasisi nyingine za kifedha hazitoi mkopo huu kwa mtu anayeanza ujenzi bali hutoa mkopo kwa mradi ambao tayari ulishaanza kujengwa lakini mradi ukashindwa kumalizika kwa sababu fedha haikutosha hivyo wanatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo. Hili huwa wanafanya hivi ili kujihakikisha kwamba mhusika tayari amejitoa kweli katika ujenzi huo na sio mbabaishaji. Hata hivyo pamoja na vigezo na masharti yote hayo taasisi nyingi za kifedha huwa na aina mbalimbali za mikopo kwa ajili ya ujenzi “mortgage”.
Karibu sana.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255 717 452 790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!