MSINGI WA JENGO UANZIE JUU.

Mara nyingi watu huwa hawajui vitu vinavyopelekea jengo kuvutia au kuwa na mwonekano fulani wa kipekee unaoleta maana. Hii ni kwa sababu mvuto au uzuri wa jengo hausababishwi na kitu kimoja pakee bali ni muunganiko wa vitu vingi vilivyofanyika kitaalamu na kwa kuzingatia kanuni fulani maalum ndio hupelekea jengo kuwa na mvuto huo wa aina yake. Muunganiko huu huhusisha kila kitu kinachooneka kwenye jengo kuanzia chini mpaka juu na kwa kuzingatia sifa zote za vipengele husika vya jengo.

Sasa moja kati ya vitu ambavyo hupaswa kufanyika kwa kuzingatia kanuni maalum na zisizotakuwa kuvunjwa kiurahisi ni urefu wa msingi wa nyumba mpaka kuifika sakafu ya chini. Kuna faida nyingi sana za msingi wa jengo kwenda juu ikiwemo mvuto wa kimuonekano. Tunaposema msingi wa jengo unapaswa kwenda juu tunamaanisha kwamba kutoka chini kwenye ardhi mpaka kuifikia sakafu ya nyumba kunapaswa kuwa na angalau mita 0.6. Urefu wa mita 0.6 za msingi unamaanisha kwamba kutapaswa kuwa na ngazi nne za kupanda mpaka mtu kufikia level ya sakafu ya chini ya nyumba.

Yapo majengo mengi ambayo hayakuzingatia eneo hili na kupelekea watumiaji wa jengo husika mara nyingi wakikutana na changamoto mbalimbali kama vile maji kuingia ndani ya nyumba kunapokuwa na mvua kubwa, vumbi na michanga kujaa ndani ya nyumba. Lakini pia msingi wa jengo unapokwenda juu unarahisisha sana huduma za ndani ya jengo kama vile uhandisi huduma, mifumo ya maji safi, mfumo wa majitaka na hata mfumo wa maji ya mvua.  Katika hali ya kawaida urefu wa msingi huo unapaswa kuonekana kwa mtu yeyote kwa idadi ya ngazi zitakazokuwepo. Kunapaswa kuwa na angalau kazi tatu kisha ya nne ndio kuingia ndani ya nyumba.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *