KUENDELEZA NYUMBA ILIYOPO NA KUCHORA RAMANI UPYA.
Katika kufanya kazi za ramani za nyumba kuna watu wengi ambao wanahitaji ramani mpya kabisa kwenye kiwanja kipya lakini kuna watu wachache ambao wao wanahitaji kuendeleza nyumba ambayo tayari ipo katika eneo husika aidha kuifanya kuwa kubwa zaidi au kuifanya kuwa ya ghorofa kabisa. Hata hivyo kazi hizi zote zinafanyika kwa namna tofauti na ile ambayo ni kuendeleza ndio huwa ina kazi kubwa zaidi na inahitaji mchakato mzito zaidi kuliko ramani ya nyumba mpya inayoanza.
Kwa nyumba ambayo ni ya kuendeleza ambacho huwa kinatakiwa kufanyika kwanza huanza na kuitembelea kisha kuipima upya na kuichora tena upya kama ilivyo. Zoezi la kuichora upya ambalo kitaalamu huwa tunaita (documentation) linaweza kuepukwa ikiwa tu ramani ya nyumba husika inaweza kupatikana tena iwe haikubadilishwa kabisa wakati wa ujenzi. Tofauti na hapo nyumba hiyo itapaswa kupimwa upya kisha kuchorwa tena upya kama ilivyo halafu baada ya hapo ndio ramani itaanza kufanyiwa mabadiliko.
Hivyo tumeweza kuona mchakato wa kuendeleza ramani ya nyumba iliyopo jinsi unahitaji kujihusisha sana na iliyopo katika kuikuza au kuiendeleza. Tukija kwenye ramani ya nyumba mpya kinachotokea ni kwamba huhitaji kabisa kushughulika na kilichopo zaidi tu ya kuangalia namna eneo inapojengwa lilivyokaa na mazingira yanayolizunguka eneo hilo na kisha kufanya kazi ya ramani kuendana na mazingira yake. Kimsingi kwa ramani mpya kabisa, ikiwa umepata maelezo ya kujitosheleza kuhusiana na eneo inapojengwa na eneo lenyewe likawa halina utata basi unaweza hata usifike katika eneo la ujenzi lakini bado ukaweza kuchora ramani sahihi kabisa.
Kwa maana hiyo kazi ya kuchora ramani ya nyumba ambayo tayari ipo lakini inaendelezwa ni kubwa zaidi au tunaweza kusema ni kazi mara mbili ukilinganisha na kazi ya kuchora ramani mpya ya nyumba ambayo haikuwepo kabisa. Hivyo kwa msanifu majengo kazi ya kuchora ramani mpya ya jengo jipya ni rahisi zaidi kuliko kazi ya kuchora ramani ya kuendeleza jengo ambalo tayari lilikuwepo.
Karibu sana kwa huduma za ramani na ujenzi.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!