UNAPIMA UJAZO WA MAGARI YANAYOLETA VIFAA VYA UJENZI KWENYE MRADI WAKO?

Watu wengi wamekuwa wanaibiwa sana sio kwa sababu ya ujanja wa wale wanaoiba bali kwa sababu ya kupenda urahisi kwa wale wanaoibiwa. Wezi wanajua kwamba watu wengi wanapenda vitu vya bei rahisi bila hata kujiuliza huo urahisi umetokea wapi, hivyo huwa wanatumia mwanya huo huo wa watu kupenda urahisi kwa kuwaonyesha kwamba wanawasaidia kumbe kimsingi wanawaibia bila hata wao wenyewe kugundua. Watu hawa wanaahidi kukufanyia kazi kwa bei rahisi sana ambayo hukuwa hata unaitegemea na wewe kuingia kwenye mtego huo bila kufikiria mara mbili mbili na hivyo unajikuta umeumizwa zaidi kinyume cha vile ulivyotegemea kwamba utapata kwa bei rahisi badala yake inakuwa ghali zaidi.

Sasa kuna mchezo ambao huwa unafanyika sana kwenye maeneo ya ujenzi hasa kwenye vifaa vya ujenzi vya ujazo kama vile mchanga, kokoto, zege n.k., ambapo kuna watu wengi watakuahidi kukuletea ujazo fulani kwa gharama nafuu. Wewe utafurahia na kuwapa hiyo kazi ya kukuletea kiasi hicho mpaka eneo la ujenzi kwa gharama hiyo na utawalipa. Sasa kama hupimi gari husika kabla na baadaa ya kumwaga vifaa hivyo kwenye eneo lako la ujenzi usibaki unashangilia kwamba umefanikiwa kununua vifaa kwa gharama nafuu, kwani huenda umeletewa vifaa pungufu kwa sababu sio idadi kwamba unaweza kuhesabu bali havitatosha na utapaswa kununua tena na tena na kujikuta ukiingia gharama kubwa zaidi ya vile ilivyostahili.

Kwa hiyo sasa haijalishi umepata vifaa kwa bei nafuu au bei ghali ni muhimu sana kupima ujazo wa yale magari yote yanayoleta vifaa kwenye eneo lako la ujenzi kwa vifaa ambavyo huhesabu kwa idadi bali kwa ujazo ili kuhakikisha kwamba unaletea kiasi ulicholipia. Hili ni jambo muhimu sana kulizingatia kwa sababu huu mchezo unafanyika kwa kiasi kikubwa sana aidha na wauzaji wenyewe au madereva ambao wanapunja ujazo mpaka kufikia kiasi ambacho kinakamilisha mzigo kamili anaoenda kuuza. Kama huna uelewa wa namna ya kupima ujazo unaweza kumtumia mtu mwingine mwenye uelewa sahihi akakusaidia kwenye hili kwa sababu utajikuta unapoteza kiasi kikubwa cha fedha kwenye wizi na kusababisha mradi wako kukugharimu pesa nyingi zaidi ya vile ulivyotegemea.

Karibu sana kwa huduma zote za ujenzi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *