Jengo Lako Ni Biashara Na Utambulisho Wako

Na Architect N. Moshi
+255717452790

Habari Ndugu

Karibu Tuendelee Kuelimishana Mambo Zaidi Kuhusu Namna Tunajenga Majengo Yetu

Ndugu mdau wa ujenzi, kitu nataka nikukumbushe leo ambacho watu wengi hawajui ni kwamba, jengo lako ni biashara

-Jengo au nyumba ni tofauti na vitu vingine, jengo huwa liko wazi linaonekana na kila na linakuwa ndio kama utambulisho wake, watu huliangalia, watalisifia sana kama ni zuri au kulikosoa sana kama halina mvuto na kuendelea kulizungumzia kila wakati. Litakuwepo kwa miaka mingi sana pengine mpaka utazeeka kabisa.

-Muonekano wa jengo lako utaleta picha ya umakini wako, kama litakuwa jengo lenye ubora na lililojengwa kwa viwango litaashiria wewe ni mtu makini, kama halitakuwa na mvuto kimuonekano na limejengwa hovyo ni ishara kwamba wewe ni mtu usiyejali

-Jengo lako linaathiri hadhi yako sifa yako mtaani, kama litakuwa ni jengo bora lenye kuvutia litaongeza sifa yako na kama litaonekana halina mvuto na thamani ya pesa haionekani litakujengea sifa mbaya

-Jengo lako linaathiri hadhi yako kijamii. Sio tu ukubwa wa mradi ndio unaashiria hadhi yako kijamii bali pia ubora wa mradi. Jengo lililobuniwa vizuri mpaka mazingira yake ya nje kisha kujengwa kwa viwango bora litaongeza hadhi yako kwenye jamii na heshima kwenye familia wakati jengo lisilowekwa kazi ya kutosha kiasi cha kutokuwa na mvuto wala ubora litapunguza sana hadhi yako katika jamii na hata heshima ndani ya ukoo na familia

-Uimara wa jengo lako ni ishara ya umakini, uchaguzi sahihi, nguvu na akili ulizoweka kufanikisha, wakati udhaifu wa jengo lako ni ishara ya uzembe na kukosa umakini katika mradi husika

-Tofauti na vitu vingine jengo/nyumba ni kitu kinachoonekana wazi, kama litakuwa zuri na lenye mvuto utalifurahia siku zote, kama litakuwa limejengwa hovyo na kukosa umakini litakukasirisha na kukukosesha raha siku zote.

N:B Jengo Lako Ni Alama Yako Na Mtazamo Wako, Hakikisha Unafanya Maamuzi Sahihi Na Kuweka Umakini Wa Kutosha Kuhakikisha Linaongeza Hadhi Na Heshima Yako Kazini, Nyumbani Na Kwa Jamii Kwa Jumla.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *