2. UJENZI WA KUTUMIA CHUMA (STEEL STRUCTURES)

-Ujenzi wa kutumia chuma hufanywa kwa kutumia chuma imara sana na yenye nguvu inayoitwa (mild steel). Chuma hizi ni imara sana kiasi kwamba ukichukua nondo yenye kipenyo(diameter) ya 1inch au 25mm unaweza kuning’iniza mzigo wenye tani 20 na inahimili. Uimara huu ni faida kubwa kwa majengo. Faida nyingine ya kutumia chuma ni urahisi wake wa kupinda bila kuvunjika au kukatika(flexibility). Pale inapotokea jengo likasukumwa kwa upepo mkali au tetemeko la ardhi huweza kupinda kidogo na kurudi bila kuvunjika wala chuma kupata changamoto nyingine yoyote aidha ya kukatika wala kupasuka. Sifa hizi pia za chuma kupinda taratibu bila kuvunjika moja kwa moja pia zinasaidia kutoa taarifa mapema kwa watumiaji wa jengo kwamba waanze kuchukua tahadhari au marekebisho yafanyike badala ya kuanguka ghafla na kuleta madhara.

Kuanguka kwa jengo la chuma aina hizi huwa halianguki kwa mara moja, majengo haya huwa yanakabiliana vizuri zaidi na tetemeko la ardhi kuliko aina nyingine nyingi kwa sababu ya sifa zake hizi za kutovunjika badala yake ni kupinda kidogo.

Hata hivyo changamoto kubwa ya majengo ya kutumia chuma ni kwamba hudhoofika kiurahisi inapotokea ajali ya moto. Joto linapofikia nyuzi joto sentigredi 500 chuma hiki(mild steel) hupoteza nusu ya uimara wake. Hiki ndicho kilichoyatokea yale majengo ya “World Trade Tower”, New York, Marekani mwaka 2001, kwenye yale mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Alqaeda maarufu kama 911 au September evelen. Kwa hiyo chuma katika majengo inatakiwa ilindwe sana dhidi ya moto au joto kali kwa kuweka gamba gumu la kuzuia moto kuifikia chuma au kufunga vuzuia moto na vizima moto katika jengo mara tu utakapojitokeza.

-AINA ZA MAJENGO AMBAPO UJENZI WAKE HUTUMIA CHUMA.

-Kwenye majengo marefu sana – kwa sababu ya uimara wake, wepesi wake na kasi ya ujenzi.

-Majengo ya viwandani – kwa sababu ya kwenda upana mrefu bila kutegemea nguzo za katikati na kwa gharama ndogo. Nguzo za katikati huua nafasi na kuleta usumbufu ndani ya jengo.

-Majengo makubwa ya kuhifadhi mizigo(godowns) – kwa sababu ya kuepuka nguzo za katikati pia.

-Majengo ya makazi – yale yanayolazimu kuwa mepesi.

-Majengo ya muda mfupi – yale yanayojengwa na kutumika kwa kipindi fulani kisha kuhamishwa kwa ajili ya matumizi mengine na eneo jingine.

AINA ZA UJENZI WA KUTUMIA CHUMA

 1. Ujenzi Chuma Saiti – Huu ni ujenzi wa kutumia chuma ambapo kazi kubwa ya kutengeneza na kuunda vifaa hivi vya chuma vinavyoenda kusimamisha jengo husika na inafanywa na timu ya watu wataalamu wa chuma au kwa kiasi katika karakana iliyopo katika eneo la ujenzi.
 2. Ujenzi Chuma Kiwandani – Hii ni aina ya ujenzi wa kutumia chuma ambapo kazi yote ya kuandaa vifaa vya chuma vinavyoenda kufungwa kwenye eneo la ujenzi inafanyika kiwandani. Baada ya hapo vifaa vyote husafirishwa kwa malori makubwa kuelekea eneo la ujenzi ambapo hufungwa moja kwa moja. Njia hii ni bora zaidi na inatumika zaidi kwa sababu kiwandani kila kifaa huweza kutengenezwa na ujenzi huenda haraka sana kutokana na kila kitu kukamilika kiwandani kisha eneo la ujenzi huwa ni kufunga moja kwa moja.

FAIDA ZA UJENZI WA KUTUMIA CHUMA

-Ni ujenzi unaotumia muda mfupi sana kukamilika hivyo inaokoa sana muda.

-Chuma hizi zinakunjika badala ya kuvunjika hivyo ni rahisi kukabiliana na nguvu za kimazingira kama upepo mkali, tetemeko la ardhi, n.k bila jengo kuathirika kwa haraka.

-Ujenzi wa chuma unarahisisha upatikanaji wa kila kifaa kinachohitajika kwani kila kifaa kinaweza kutengenezwa kiwandani.

-Upatikanaji wa kila umbo linalohitajika kuendana na jengo linavyotaka na kuweza kubandikwa urembo mwingine wowote wa kubandika kiurahisi.

-Upatikanaji wa vifaa vingi tofauti tofauti vya kufungua kama bolti, nati, kuchomea au kugongelea.

CHAGAMOTO ZA UJENZI WA KUTUMIA CHUMA.

-Chuma zikikumbwa na joto kali sana hudhoofika na pia ni rahisi kushika moto.

-Katika mazingira ya unyevu na ndani ya maji chuma ni rahisi kushika kutu.

Na Architect Sebastian

+255717452790

1 reply
 1. SUNBANK MABATI
  SUNBANK MABATI says:

  We are Great City Material Tanzania Limited ( with brand name `SUNBANK`) , We
  are dealing in manufacturing of Iron sheet and other construction material ,We are
  registered with Tin Number 137-861-909 , Located in Ungalimited , Industrial Area ,
  Block E , Plot Number 94 , Arusha and Branch in Dar es salam, Ilala Vingunguti ,
  Plot Number 5. We are dealing with the best quality roofing sheet products with
  different Gauge 30,28 and 26 of different width 110 cm and 90 cm. Therefore we
  present to you a business proposal , which will mutually benefit both parties and
  enable you to use our best quality roofing products.
  Our company is therefore willing to supply roofing sheets and other materials
  ( Roofing nail) to your good office with a competitive price , approved quality with
  five years warranty and the shortest production time.
  It is our great hope that you will consider our company to cooperate with you.
  Attached with this letter you will find a copy of big projects which we have already
  supplied with our products in the market .

  TERMS OF DELIVERY
  1. 50% BEFORE DELIVERY AND THE AMONOUNT REMAIN WILL BE PAYED AFTER DELIVERY
  2. LOCAL PURCHASING ORDER (L.P.O)
  3. FULL PAYMENT
  Yours Faithfully
  ….………………..
  FRANCIS JOSEPH
  CORPORATE SALES
  +255 754 471 453.
  GREAT CITY MATERIAL TANZANIA LIMITED

  Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *