3. UJENZI WA KUTUMIA CHUMA NYEPESI(LIGHT GAUGE STEEL CONSTRUCTION)

Ujenzi wa kutumia chuma nyepesi ni aina ya ujenzi ambao chuma ndogo ndogo nyepesi zinapangiliwa kutengeneza pande zote za jengo. Chuma ndogondogo nyepesi zinafungwa karibu karibu kutengeneza kuta na paa la jengo husika. Kisha wanazifunganisha kwa kutumia paneli za chuma, bati au paneli nyingine.

>

Mara nyingi chuma hizi huandaliwa na kutengenezwa kiwandani zikiwa tayari kabisa kufungwa maeneo husika ambapo mafundi wanaozifunga hutumia nyundo maalum na misumari yake.

Mfumo huu hutumika pia katika kugawanya maeneo ya ndani ya jengo kwa matumizi tofauti tofauti(interior partitions) na kimsingi mwanzoni lengo lake maalum zilitengenezwa kwa matumizi ya ndani kugawanya vyumba.

FAIDA ZA UJENZI WA KUTUMIA CHUMA NYEPESI

-Kwanza ni nyepesi, ambapo zinaharakisha ujenzi bila kutumia mashine na vifaa vizito. Kila kitu kinabebwa kiurahisi na mikono na kazi ya kufunga inakuwa kama kazi ya useremala kwa uwingi. Kazi kubwa ni kupanga chuma sehemu sahihi na kuifunga kwa skruu kwa kutumia nyundo maalum ya skruu.

-Chuma hizi zinaweza kuwekwa katika umbile lolote na zinaweza kuwekwa aina yoyote ya vifaa juu yake kwa muonekano bora wa mwisho.

-Ni rahisi kufanya mabadiliko katika jengo husika muda wowote kiurahisi kabisa.

-Ujenzi wa kutumia chuma nyepesi unaendana na mifumo mingi ya kiujenzi na aina nyingi ya huduma ndani ya majengo.

-Chuma hizi nyepesi pia haziruhusu moto hovyo ambalo ni hitaji muhimu kwa baadhi ya majengo.

-Chuma nyepesi haziozi, kusinyaa au kuharibika umbo kwa ajili ya joto kali kama ilivyo mbao na kutoruhusu wadudu hatari kama vile mchwa ambao ni hatari kwa majengo.

CHANGAMOTO ZA UJENZI WA KUTUMIA CHUMA NYEPESI

-Chuma nyepesi zinaruhusu sauti kupenya kiurahisi zaidi ukilinganisha na kutumia zege katika kujenga.

-Moto ukikamata eneo jingine la nyumba na kuwa mkubwa kiasi cha kuathiri chuma nyepesi hudhoofika na kuweza kusababisha jengo kuanguka.

Na Architect Sebastian Moshi

+255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *