5. UJENZI WA JENGO LINALOBEBWA NA KUTA

5. UJENZI WA JENGO LINALOBEBWA NA KUTA

Hii ni aina ya ujenzi ambayo imetumika sana kwa majengo ya ghorofa miaka ya 1700 mpaka 1900 mzigo wote wa jengo unabebwa na kuta za jengo badala ya nguzo na boriti(beams). Siku hizi aina hii ya ujenzi haitumiki tena isipokuwa kwa majengo madogo ya makazi na ni kwa uchache sana.

Badala yake siku hizi majengo marefu yanajengwa kwa kutumia mihimili ya majengo kama vile nguzo na boriti na kuta zake huwa nyepesi, nyembamba na wakati mwingine kuta za vioo nje na ndani ya jengo.

Kwa Nini Aina Ya Ujenzi wa Kuta Kubeba Jengo Hautumiki Tena?

-Ujenzi huu wa kuta kubeba jengo hautumiki tena kwa sababu kwanza ni rahisi kuathiriwa na tetemeko la ardhi. Vifo vingi vilivyotokana na tetemeko la ardhi vimetokea kwa majengo yanayobebwa na kuta.

-Ujenzi wa kutumia kuta unajengwa kwa mikono hivyo unahitaji wafanyakazi wengi sana kwa sababu hautumii mashine kama mihimili kitu kinachosababisha hata ujenzi wake kwenda taratibu sana.

-Majengo yanayobebwa na kuta huwa ni mazito sana na yanategemea malighafi nyingi sana kwani kuta zake huwa nene na zilizoshikana sana ili kusaidia jengo kuwa imara.

Majengo mengi ya miaka ya zamani yalijengwa kwa aina hii ya ujenzi ya kuta kubeba jengo lakini kuanzia karne ya 20 ujenzi hasa wa majengo marefu umekuwa ukifanywa kwa mihimili kubeba jengo na unatumia zaidi teknolojia za kisasa na kurahisisha ujenzi.

Na Architect Sebastian Moshi

+255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *