UJENZI WA KUTUMIA MBAO NYEPESI.

Ujenzi wa kutumia mbao nyepesi ni aina ya ujenzi ambao unafanyika sana baadhi ya maeneo duniani hasa Amerika na Ulaya.

Ujenzi wa kutumia mbao nyepesi una sifa zifuatazo

-Ni nyepesi na unaruhusu ujenzi wa haraka, bila kuhusisha vifaa vizito. Vifaa vyote vinabebwa tu kwa mikono, ujenzi unakuwa kama kazi kubwa ya useremala. Kifaa kikuu ni nyundo ya kisasa ya kufungia misumari mithili ya bunduki.

-Ujenzi wa mbao unaweza kuwekwa katika umbile lolote na kufunikwa juu kwa aina yoyote ya vifaa vya umaliziaji kama vile ubao vigae, aluminium, pvc, kioo n.k.

-Bidhaa nyingi na mifumo mingi katika ujenzi inaweza kuendana na ujenzi wa mbao nyepesi.

Changamoto zake

-Zinaweza kushika moto kiurahisi na ukapata nguvu haraka kwa sababu ni mbao.

-Mara nyingi hushindwa kukabiliana na upepo mkali kama vile kimbunga n.k.

AINA ZA UJENZI WA KUTUMIA MBAO NYEPESI

  1. MIHIMILI YA MBAO NYEPESI ZA MOJA KWA MOJA – Hii ni aina ya ujenzi wa kutumia mbao nyepesi ambapo ambapo zile mbao zinaanzia kwenye msingi na kwenda moja kwa moja mpaka ghorofa ya kwanza, hivyo ule mfumo wa mihimili unakuwa unategemeana kutoka chini mpaka juu. Aina hii ya ujenzi haitumiki tena kwa sababu kwanza huwa nzito sana kunyanyua huo ukuta wa mbao kuanzia chini mpaka ghorofa ya kwanza. Pili pale inapotokea hitilafu jengo likashika moto huwa rahisi kuambukiza kutoka kwenye ghorofa ya chini mpaka ya juu moja kwa moja kwa sababu imeunganishwa, hivyo kuwa na mdhara makubwa ndani ya muda mfupi.
  •  MIHIMILI YA MBAO NYEPESI ZINAZOJITEGEMEA KILA SAKAFU – Hii ni aina ya ujenzi wa kutumia mbao nyepesi ambao kila sakafu(floor) inajengwa na kumalizika kisha ndipo sakafu(floor) nyingine inafuata na mwisho kupauliwa. Ujenzi wake huo mwepesi kwa sababu mbao zake ni fupi hivyo zinakuwa rahisi kubebeka na kuzijengea kwa sakafu(floor) husika. Pia unapotokea moto hauwezi kwenda moja kwa moja hivyo unapoudhibiti unakuwa bado haujaleta athari kwenye sakafu(floor) nyingine.

Mawazo ya kujenga jengo kwa kutumia mbao nyepesi yalianza kutumika miaka kama 100 iliyopita baada ya wajenzi waliokuwa wanafanya kazi ya kugawa vyumba ndani ya majengo makubwa kwa kutumia mbao nyepesi kupata mawazo kwamba mbao nyepesi zinaweza kutumika zenyewe kujenga jengo zima bila kutumia matofali na cement.

Hata hivyo kwa zama hizi ujenzi wa kutumia mbao nyepesi unaenda ukipungua na badala yake ujenzi wa chuma nyepesi kama tulivyojadili hapo huu unaendelea kuchukua nafasi yake.

Na Architect Sebastian Moshi

+255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *