6. UJENZI UNAONZIA KIWANDANI(PRECAST CONCRETE CONSTRUCTION)

Ujenzi Ulioanzia Kiwandani Kuelekea Saiti

Ujenzi unaoanzia kiwandani ni aina ya ujenzi ambao vifaa vya ujenzi vinatengenezewa eneo jingine tofauti na eneo jengo linapojengwa. Vifaa vikishatengenezwa vinasafirishwa kwenda eneo la ujenzi kisha kufungwa. Hii ni tofauti na ujenzi wa kawaida ambao kila kitu kinafanyikia eneo jengo linapojengwa.

FAIDA ZA UJENZI UNAONZIA KIWANDANI

Ujenzi unaonzia kiwandani hurahisisha kazi ya ujenzi kama ifuatavyo

-Ujenzi wote hufanyikia chini badala ya juu sana kutoka ardhini hivyo kupunguza hatari nyingi.

-Ujenzi unaweza kufanyikia kwenye eneo la ndani hivyo kuepuka kuathiriwa na hali mbaya ya hewa inayoweza kuharibu au kuchelewesha kazi.

-Mifumo inayotengeneza vifaa na maumbo katika ujenzi inaweza kutumika mara nyingi sana hivyo kupunguza gharama ya muda na vifaa ya kujenga na kubomoa kila wakati.

-Vifaa vya kisasa vinavyoweza kuboresha sana kazi vinaweza kutumika.

-Kunyweshea ili kuimarika zege kunaweza kufanyika katika umakini mkubwa na kufanikisha ubora wa hali ya juu.

-Kazi ya ujenzi inaweza kufanyika kwa haraka sana na kuokoa muda mwingi ukilinganisha na ujenzi unaofanyika site ambao unahitaji kwenda hatua kwa hatua ikisubiri hatua moja ikamilike ndio nyingine ifuate.

CHANGAMOTO ZA UJENZI UNAONZIA KIWANDANI

-Hakuna muunganiko wa baadhi ya sehemu za jengo kama nguzo hivyo inahitaji umakini mkubwa kuhakikisha jengo haliathiriki na changamoto ya kimihimili.

-Kwa sababu jengo haliunganiki moja kwa moja katika mihimili yake litahitaji kuwekwa vifungashio maalum katika miunganiko yake vitakavyozuia maji kupenya na kuingia ndani ya jengo.

-Kutahitajika mashine nyingi za winchi ambazo zitakuwa zinafanya kazi katika jengo zima kwa sababu vifaa vyote vya jengo zima vitakuwa vinafungwa kwenye jengo kutokea kiwandani moja kwa moja.

NAMNA NA MAHALI AMBAPO UJENZI UNAOANZIA KIWANDANI HUTUMIKA.

-Hutumika kutengeneza boriti, nguzo, sakafu za zege, msingi na vipengele vingine vya kiuhandisi.

-Hutumika kutengeneza kuta na vibao vingi vinavyowekwa katika kuta za jengo.

-Hutumika kutengeneza maumbo mbalimbali ya aina tofauti yanayohitajika katika kukamilisha jengo.

-Hutumika kutengeneza vifaa na sehemu za ujenzi katika ujenzi wa vitu mbalimbali kama vile madaraja marefu.

-Hutumika kutengeneza vifaa vya ujenzi vinavyouzwa kama vile mabomba, matenki ya maji, tailizi za sakafu, kuta n.k.

Na Architect Sebastian Moshi

+255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *