7. (JENGO LINALOJENGWA KIWANDANI) PRE-ENGINEERING BUILDINGS

Jengo Linalojengwa Kiwandani

-Ujenzi wa jengo linalojengwa kiwandani ni ile hali ya mkandarasi kwenda kufanyia ujenzi wake kiwandani kisha kulisafirisha mpaka saiti eneo na kulifunga. Tofauti ya ujenzi unaonzia kiwandani na jengo linaloanzia kiwandani ni kwamba ujenzi unaoanzia kiawandani mkandarazi anaweza kuagiza atengenezewa kitu cha umbo fulani kiwandani kisha kupelekewa saiti lakini jengo linaloanzia kiwandani mkandarasi mwenyewe ndio anaenda kulijengea huko kiwandani kisha anasafirisha sehemu zake mpaka saiti na kulifunga baada ya kuwa msingi na sakafu ya chini vimekamilika.

-Ujenzi huu wa jengo kujengwa kiwandani huwa wa kasi sana kwani msingi na sakafu ya chini pamoja na matoleo huanza hata wakati maeneo mengine ya jengo yakifanyikia kiwandani na baada ya kuletwa ni kufunga na jengo kukamilika.

-Wakishafikisha jengo site hunyanyuliwa na winchi kila kipande sehemu yake kisha watu kufunga kwa bolti na nati maeneo yanayotakiwa kufungwa hasa katika boriti na nguzo za chuma.

Na Architect Sebastian Moshi

+255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *