8. UJENZI UNAOTUMIA MAROBOTI(ROBOTIC BUILDING CONSTRUCTION)

Watu mbalimbali pamoja na kampuni nyingi duniani zinaendelea kufanya na mchakato wa kutengeneza mfumo wa kutumia maroboti katika ujenzi wa nyumba. Japo hili ni jambo linalofuatiliwa na watu wengi kwa ukaribu lakini bado lina changamoto nyingi kuweza kufanikiwa kwa ufanisi unaohitajika.

Ujenzi Kutumia Maroboti

FAIDA ZA KUTUMIA MAROBOTI KATIKA UJENZI

-Kwanza maroboti yanaweza kujenga kwa ufanisi na usahihi mkubwa zaidi.

-Maroboti yanaweza kufanya kazi masaa 24, siku saba za wiki bila kujali hali ya hewa au mazingira.

-Maroboti yanaondoa namna zote za uzembe na matatizo yanayoweza kuletwa na watu katika ujenzi kama utoro, uchelewaji, ulevi, makosa, uvivu, ajali, ulazima wa usalama, ulazima wa bima za afya, kutokuelewana na ugomvi baina ya wafanyakazi n.k.,

-Maroboti yanaweza kufanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi kwa binadamu kama vile maeneo yasiyo na hewa, gizani, kwenye veranda za majengo marefu sana bila hofu, woga, kuhisi kizunguzungu wala kujali.

-Maroboti hayawezi kutengeneza vyama vya wafanyakazi au umoja na kufanya migomo kudai nyongeza au maslahi mengine kama ilivyo kwa watu au binadamu wa kawaida.

Sababu zote hizi zinafanya maroboti kutegemewa zaidi na kuwa na nafuu kubwa zaidi katika ujenzi kuliko watu na yanaweza kuwa na manufaa zaidi siku zijazo.

Na Architect Sebastian Moshi

+255717452790

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *