9. UJENZI WA JENGO KWA KUTOA NAKALA ZA 3D(3D’s PRINTING BUILDINGS)

JENGO LILILOJENGWA KWA 3D PRINTING

Hii ni aina ya ujenzi ambayo mashine inaunganishwa kwenye computer ambapo mchoro wa jengo unasoma kisha zile mashine kama maroboti zinaanza kazi ya kujenga jengo husika kama vile mtu anavyotoa nakala(ku-print) maandishi ambayo yapo katika nakala tete na kutoa karatasi kwenye printer bila mtu kuigusa mashine kwa mkono. Katika ujenzi wa aina hii mashine ikishaunganishwa kwenye kompyuta na mchoro husika kusetiwa moja kwa moja zinaanza kazi za kujenga jengo husika kama lilivyo kwenye mchoro mpaka kukamilika. Hii teknolojia ambayo tayari imeanza kufanya kazi baadhi ya maeneo kwa kiasi kidogo lakini matumizi yake kamili kabisa bado yanafikiriwa yatachukua muda mrefu sana.

Na Architect Sebastian Moshi

+255717452790

Tembelea www.ujenzimakini.com, kwa huduma zetu sambamba na kufahamu zaidi

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *