AINA ZA MAWE ZINAZOTENGENEZA VIGAE VYA SAKAFU NA KUTA(FLOOR AND WALL TILES)

Malighafi zinazotokana na mawe hutengeneza sakafu nzuri(floor finishes) na nyingi bei zake ni nzuri pia. Malighafi zinazotokana na mawe au miamba zina faida zake nyingi ambazo hazipatikana kwa vigae(tiles) zinazotengenezwa kwa mchanganyiko wa udongo na mchanga kama vile tailizi za ceramic au porcelain.

AINA ZA MALIGHAFI ZA MAWE AU MIAMBA

  1. GRANITE

Aina za mawe/miamba za granite ambazo hutengeneza vigae vya sakafu na kuta ni mawe ambayo kwa asili yametokana na miamba ya volcano iliyotokana na milipuko ya lava kwa mamilioni ya miaka iliyopita.

Sifa za mawe au miamba hii aina ya granite:

-Ni migumu, imara na haipukutiki kiurahisi wala kumonyonyoka baada ya kukanyagwa sana.

-Haiathiriwi na kemikali za tindikali(acids)

-Inaweza kupakwa rangi za silk na ikawa na uso laini unaong’aa kama kioo.

Sifa hizi zinaifanya granite kuwa sahihi sana kwa matumizi ya kwenye sakafu pamoja na kwenye kumalizia kaunta za jikoni, bar n.k. Mawe au miamba hii ya granite inafaa sana pia kubandika ukutani juu ya ukuta wa kawaida katika kumalizia ukuta au finishing.  Hata hivyo mara nyingi granite zinapatikana katika rangi zisizo na mwanga sana kama nyeusi, nyekundu, kijivu na kwa nadra sana unaweza kupata nyeupe. Upatikanaje wake katika rangi hizi zisizo na mwanga sana unaizuia kutumika baadhi ya maeneo ambayo yanahitaji rangi zenye uwezo mkubwa wa kuakisi mwanga.

Uso wa granite pia unaweza kufanyiwa kazi na ukawa na mwonekano wa tofauti na laini au unaoteleza. Unaweza kupigwa maji ya presha, au mchanga au kuchanjwa na kutengeneza uso ambao uko rafu ambao ni muhimu kwa matumizi ya maeneo ya nje au outdoors, kwenye vibaraza au kwenye njia za watembea kwa miguu. Mawe maarufu yaliyokuwa yanatumika karne za nyuma sana yanayojulikana kama “cobblestone” nayo yalikuwa ni ya aina ya granite.

Na Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

Kupata maarifa bora ya ujenzi ingia kwenye website yetu www.ujenzimakini.com

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *