2. MARBLE, Tanzania

Malighafi ya Marble ni aina ya mawe au miamba iliyotokana na mwamba moto(metamorphic rock). Mwamba moto ni mwamba uliotengenzwa kutokana na msukumo mkubwa wa presha na joto  kali huko ndani kabisa ya ardhi ya dunia.

Tailizi Marble

Sifa Za Mawe au Miamba ya Marble

-Marble ina uso laini na inaporomoka pale inaposuguliwa sana

-Marble inaathiriwa na kemikali za tindikali au acids

-Inaweza kupakwa rangi au polish na kung,aa kama kioo.

-Marble inapitisha mwanga kidogo sana kwa taabu sana translucent.

Kwa maana hiyo marble hazifai kutumia kwenye maeneo ya umma au maeneo yanayopitiwa na watu kwa wingi sana kama vile kwenye baraza za kuingilia, kwenye ngazi za kwenye maeneo ya umma n.k., maeneo hayo yanafaa zaidi kutumia granite. Kwa sababu inaathiriwa na acids marble haifai kutumika maeneo yenye acids kama kwenye maliwato za kukojolea kwa sababu mikojo ina acis, lakini pia jikoni ambapo kuna matunda yenye acids kama malimao n.k., Lakini marble inangaa na kupendeza sana na pia inaleta hisia za hamasa sana unapoikanyaga. Marble inapatikana kwa rangi nyingi sana hasa rangi zenye kuwakawaka.

Tiles za Marble

Na Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *