SANDSTONE OR QUARTZITE

Malighafi ya sandtone au quartzite ni aina ya mawe au miamba iliyotona na mwamba tabaka[sedimentary rocks}. Mwamba tabaka ni mwamba uliotengenezwa kutokana na mlimbikizo mkubwa wa malighafi za ardhini kama udongo, mchanga, mimea n.k., kwa mamilioni ya miaka.

Paving za Sandstone

Sifa za Sandstone.

-Haipukutiki au kumomonyoka kirahisi inapokanyagwa sana japo inategemea na namna ilivyokatwa kwa sababu iko katika matabaka hivyo kama imekatwa bila kuzingatia unene wa tabaka inaweza kuwa dhaifu

-Haiathiriwi kiurahisi na kemikali za tindikali za acids

-Ina uso ambao uko rafu sana hivyo haiwezi kupakwa rangi ikaleta mngao kama wa kioo  kama ilivyo kwa Marble na Granite.

Jiwe la Sandstone

Sifa hizi zinaifanya sandstone kufaa zaidi kwa matumizi ya maeneo yanayokanyagwa sana na maeneo ya nje kwa ujumla kwa sababu hazitelezi. Sandstone pia inafaa sana kwa matumizi ya kwenye maeneo ya mauzo kwa sababu ya utofauti wake na granite na marble. Kampuni maarufu ya teknolojia duniani kutoka Marekani ya Apple waliamua kuitumia rasmi katika kufanya finishing ya maduka yao ya bidhaa za Apple.

Na Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

Kupata makala bora za ujenzi tembelea tovuti yetu www.ujenzimakini.com

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *