SAKAFU YA PVC.

Sakafu ya pvc ni aina ya askafu inayotengenezwa na aina ya malighafi za kiwandani zinazojulikana kama vinyl.

SAKAFU YA PVC

FAIDA ZA SAKAFU ZA PVC.

-Zinaweza kupatikana katika aina tofauti tofauti za rangi na kwa ubunifu mbalimbali.

-Ni nyepesi na zinadumu muda mrefu sana

-Hazipitishi maji na hazitelezi pia hivyo zinafaa kutumika pia maeneo yenye majimaji kama vile bafuni

-Ni laini na zinamfanya ntu kujisikia vizuri anapozikanganya

-Ni rahisi kusafisha na kuziweka katika hali ya usafi na umaridadi muda wote.

CHANGAMOTO ZA SAKAFU ZA PVC

-Ni rahisi kushika moto na zinatoa moshi wenye kemikali mbaya.

-Wakati mwingine hutoa harufu isiwe nzuri zikipata joto kali hata la jua.

-Hazina uwezo mkubwa wa kukabiliana na kemikali hatari

-Zinaweza kuharibika kiurahisi kama sakafu ya chini yake sio laini

-Vitu vyenye ncha kali vinapoidondokea ni rahisi kuiharibu.

SAKAFU YA PVC

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *