SAKAFU YA ZULIA/CARPET FLOORING

Hii ni aina ya sakafu ambayo hufunikwa kwa zulia ua carpet iliyotengenezwa kwa malighafi ya nguo, kava ngumu au pamba nzito.

Sakafu Ya Zulia

FAIDA ZA SAKAFU YA ZULIA/CARPET FLOORING

-Skafu ya Zulia huhifadhi joto hivyo kwa nyakati za baridi hasa kwa maeneo yenye baridi kali sakafu ya zulia huweza kuhifadhi joto kuliko aina nyingine yoyote ya sakafu.

-Sakafu ya zulia hutengeneza mazingira sahihi zaidi ya kukaa kuliko aina nyingine ambazo ni ngumu.

-Sakafu ya zulia ni salama zaidi kwa kuwa hazitelezi n ahata ikitokea mtu ameanguka anakutana na zulia hivyo hapati maumivu sana kitu kinachoifanya zulia kuwa sahihi zaidi kwa matumizi ya nyumbani ambako kuna watoto wadogo.

-Sakafu ya zulia inaweza kupitikana kwa staili nyingi sana kwa rangi nyingi sana hivyo kutoa nafasi kwako mtumiaji kuamia aina yoyote unayoitaka na rangi yoyote unayoitaka wewe binafsi na ukafanikisha kuipata.

-Sakafu ya zulia inaondoa kabisa kelele zinazotokana na misuguano na hata yenyewe inazuia na kupunguza kelele nyingine zinazotokana na vitu kama televisheni, kompyuta, mizika n.k,

CHANGAMOTO ZA SAKAFU YA ZULIA.

-Sakafu ya zulia huwa ni changamoto sana kuisafisha pale inapokuwa imechafuka.

-Sakafu ya zulia inakamata uchafu kiurahisi na kuhifadhi na sio rahisi sana kuundoa mara moja.

-Kwa kawaida sakafu ya zulia haidumu muda mrefu sana ukilinganisha na aina nyingine za sakafu.

-Kasi ya ubunifu na mabadaliko ya sakafu ya zulia ni ndogo sana ukilinganisha na kazi ya ubunifu na mabadiliko ya aina nyingine za sakafu.

Sakafu Ya Zulia

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *