SAKAFU YA LINOLEUM

Sakafu ya linoleum ambayo mara nyingi huitwa kwa kifupi lino ni aina ya sakafu ambayo hutengenezwa kwa malighafi mbalimbali kama vile mafuta yaliyogandishwa ya linseed yanayoitwa kwa kifupi linoxyn kwa mchanganyiko na malighafi nyingine kama makoko ya miti, kemikali, unga wa mbao, madini ya canvas n.k., ambapo pingili za rangi huongezwa ili kupelekea rangi inayotarajiwa.

Sakafu Ya Linoleum

FAIDA ZA SAKAFU YA LINOLEUM

-Inadumu miaka mingi sana, ina uhakika wa kudumu mpaka miaka 25 na ikitunzwa vizuri inadumu zaidi ya miaka 40 ikiwa katika ubora wake.

-Inatengenezwa kwa malighafi ambazo zinaweza kutumika tena.

-Haina kemikali zenye sumu na haitoi harufu mbaya hata ipokutana na joto kali.

-Sakafu ya linoleum huendelea kuwa na muonekano wake bora kwa muda wote kwa sababu rangi yake haipauki kirahisi kwani tofauti na sakafu nyingi, rangi kwenye linoleum inachanganywa kwenye linoleum yote mpaka kwa ndani kabisa.

-Sakafu ya linoleum haihitaji matunzo makubwa sana zaidi ya kuisafisha kwa kufagia na kuideki mara chache.

CHANGAMOTO ZA SAKAFU YA LINOLEUM

-Sakafu ya linoleum huweza kutoboloewa na soli za kiatu chenye ncha kali au vitu vingine vyenye ncha kali.

-Linoleum huweza kubadilika kuwa nyeusi au manjano inapopigwa na jua kali hata hivyo ikiweza kuwekewa ganda maalum la juu kiwandani la kuzuia kuathiriwa na jua bado inaweza kuwa salama.

-Sakafu ya linoleum huwezi kuathiriwa na unyevu au majimaji na haishauri sana kwenye maeneo kama bafuni.

-Sakafu ya linoleum inapokuwa mpya wakati mwingine huwezi kuwa inateleza.

Sakafu Ya Linoleum

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *