AINA ZA KUTA

Kuna Aina Kuu Mbili za Kuta

  1. Kuta zinazobeba mzigo wa jengo.
  2. Kuta zisizobeba mzigo wa jengo.
KUTA ZILIZOBEBA MZIGO WA JENGO

-Kuta Zinazobeba Mzigo wa Jengo – Hizi ni aina za kuta ambazo ni sehemu ya mhimili wa jengo, kuta hizi haziwezi kubomolewa na jengo likabaki limesema, ni kuta ambazo zikibomolewa jengo litayumba na mwishowe kuanguka.

-Kuta Zisizobeba Mzigo wa Jengo – Hizi ni aina ya kuta ambazo kazi yake kubwa ni kugawa na kutengeneza vyumba lakini hata ukiondolewa jengo bado linabaki limesimama kwa hazihusiki katika kuimarisha mhimili wa jengo au sio sehemu ya mfumo wa mhimili wa jengo.

Ni vigumu kwa mtu ambaye sio mtaalamu wa uhandisi wa mihimili ya majengo kuweza kutofautisha kati ya kuta zinazobeba mzigo wa jengo na zile zisizobeba mzigo wa jengo bila ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mhandisi wa mihimili ya majengo mwenye uzoefu.

Majengo mengi ya ghorofa ya zamani hasa karne ya 19 yalikuwa yanategemea kuta kubeba mizigo ya jengo lakini hata hivyo mengi hayakuwa ni majengo marefu sana.

KUTA ZISIZOBEBA MZIGO WA JENGO

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *