MADIRISHA YA ALUMINIUM

Malighafi ya aluminium ni nyepesi na imara na sahihi sana kwa kutengeneza madirisha. Aluminium haiathiriwi na unyevu kama ilivyo kwa mbao wala kuharibika kwa kujikunja kutokana na joto kali.

DIRISHA LA ALUMINIUM

FAIDA ZA MADIRISHA YA ALUMINIUM

-Yanadumu kwa muda mrefu sana, madirisha ya aluminium yana uimara wa kudumu kwa miaka 30 mpaka 50 na hata zaidi bila kuharibika kwa sababu hayaathiriwi na hali za hewa kama baridi kali au joto.

-Yanachukuwa eneo dogo sana la fremu ya dirisha, madirisha ya aluminium kwa kawaida huchukua sehemu kidogo sana ya dirisha huku eneo kubwa likichukuliwa na paneli ya kioo jambo ambalo huruhusu mwanga mkubwa zaidi ndani ya chumba kurahisisha mtu aliyeko ndani ya chumba kuangalia mandhari ya nje vizuri sana. Hii ni tofauti na aina nyingine za madirisha kama vile Vpvc.

-Urahisi wa kutengeneza maumbo tofauti, aluminium inaweza kusaidia kuja na ubunifu wa aina nyingi kutokana na urahisi wake wa kukunjika na kukata kwa kila namna na uimara wake unasaidia pia kutengeneza madirisha na uwazi mkubwa sana.

-Rahisi kusafisha, madirisha ya aluminium huwa rahisi sana kuyasafisha na kurudi kuwa kama mapya tena.

-Yanatoa ulinzi na usalama wa kutosha kutokana na uimara wake.

DIRISHA LA ALUMINIUM

CHANGAMOTO ZA MADIRISHA YA ALUMINIUM

-Gharama, madirisha ya aluminium yana gharama kubwa ukilinganisha na madirisha ya aina nyingine ya malighafi kama vile baadhi ya mbao au Upvc.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply to Ujenzi Makini Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *