ZULIA/CARPET LA KUZUIA MAJI NA UNYEVU KWENYE JENGO(WATERPROOFING MEMBRANE)

-Zulia la kuzuia maji ni kifaa au “material” nyembamba sana inayotandazwa kwenye zege. Tabaka hili la zulia limeenea kote na haliruhusu maji kupenya kuingia ndani zaidi ya zege.

ZULIA LA SHUKA PANA YA PLASTIKI INAYOVIRINGISHWA KWENYE ROLA

ZIKO AINA MBILI ZA MAZULIA HAYA YANAYOWEKWA NDANI YA ZEGE ILI KUZUIA MAJI KUPENYA NA KUVUJA KATIKA JENGO.

-Aina ya kwanza ni Zulia kama shuka pana la plastiki linalotandazwa juu ambalo mara nyingi hupelekwa kwenye site ya ujenzi likiwa limeviringishwa kwenye rola. Mazulia haya hukatwa na kuunganishwa ili kuenea kwenye eneo zima. Mazulia mengine ya plastiki huunguzwa na kuyeyuka kidogo kwenye maungio ili kuweza kushikana vizuri kwa usahihi ili kuondoa kabisa uwezekano wa maji kupenya.

-Aina ya pili ni zulia linatengenezwa kupitia kimiminika(liquid material) kinachomwaga au kupuliziwa(spraying) kama tabaka juu ya uso husika wa zege na kutengeneza tabaka kama zulia la plastiki. Kimiminika hiki(liquid material) hutengeneza zulia ambalo halina maungio tofauti na zulia linalokuja kwenye eneo la ujenzi likiwa limeviringishwa kwenye rola ambalo litahitaji kukatwa ili kuunganishwa. Kadiri kimiminika hiki kinavyomwagwa kwa wingi kwenye eneo hilo ndivyo kinavyotengeneza zulia pana zaidi.

ZULIA LA KUZUIA MAJI LINATOKANA NA KIMIMINIKA(LIQUID BASED MEMBRANE)

-Zulia linalotengenezwa na kimiminika linaonekana kuwa bora zaidi kutokana na kutokuwa maungio ambayo huwepo kwenye mazulia yanayofika kwenye eneo la ujenzi yakiwa kwenye rola ambapo kama hayajaunganishwa kwa ustadi mzuri huwa ni maeneo dhaifu yanayoweza kuruhusu maji kupenya.

SIFA ZINAZOPASWA KUWEPO KWA MAZULIA YA KUZUIA MAJI KUVUJA KWENYE JENGO.

-Mazulia haya yanapaswa kuwa na uwezo wa kukabiliana na miale mkali ya jua bila kuathiriwa.

-Mazulia haya yanapaswa kuwa na uwezo wa kuvutika bila kukatika. Yanapaswa kuwa na uwezo wa kuvutika ikiwezekana kufika hata mara mbili mpaka tatu zaidi ya hali yake ya kawaida. Hii ni kwa ajili ya kuweza kutumiaka kwenye majengo marefu ambayo hujivuta wakati wa upepo mkali hivyo  yanapaswa kutokatika au kuchanika yanapolazimika kuvutika kutokana na mitikisiko ya jengo.

-Baadhi ya mazulia hutakiwa kuwa na uwezo wa kuruhusu mvuke kupenya.

-Mazulia haya yanapaswa kuwa na uwezo mkubwa wa kutochanika kiurahisi hata baada ya mikwaruzano na misuguano au nguvu kubwa kiasi ikitumika kuyalazimisha.

-Mazulia haya yanapaswa kuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na kemikali mbalimbali zinazoweza kuyaharibu.

-Mazulia yanayotumika kwenye ujenzi wa visima vya maji yanapaswa kuwa salama kwa chakula kwani maji haya ambayo hutumika kwa matumizi ya nyumbani yanagusana na mazulia haya.

ZULIA LA KUZUIA MAJI LINATOKANA NA KIMIMINIKA(LIQUID BASED MEMBRANE) LIKITUMIKA KWENYE SWIMMING POOL

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *