SIFA ZA MALIGHAFI ZA UJENZI

-Kudumu kwa muda mrefu, malighafi za ujenzi zinapaswa kudumu muda mrefu kwa maana ya kwamba hazitakiwi kuwa katika hali ya kushambuliwa kiurahisi na kemikali au aina yoyote ya uharibifu inayoweza kuziletea madhara katika mazingira zilizopo kama vile miale ya jua, unyevu, mvua, kutu, kupauka n.k.,

Uimara wa malighafi zinahimili changamoto za kimazingira na kudumu kwa mamia ya miaka

-Uimara, malighafi za ujenzi zinapaswa kuweza kuhimili aina zote za misukumo na presha za nje kama vile upepo mkali wa eneo husika, mvua, pamoja na malighafi nyingine zilizobebwa na jengo husika kama vile chuma, zege lililoning’inia, mabomba, reli, n.k. Zinatakiwa pia kuweza kuhimili mizigo inayobebwa kuanzia mizigo ya kuhamishika(live loads) mpaka ile isiyohamishika(dead loads).

-Zinatakiwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na mipasuko, kuchimbika, kutoboka na kuchanika. Hili unaweza kulijua kwa kuyajaribu malighafi husika kwa njia mbalimbali. Kwa mfano unaweza kulidondosha tofali kutoka juu kuona namna linavyovunjika ili kutambua uimara wake, lakini unaweza kukwangua aina tofauti za malighafi yanayofanya kazi moja kama vile marble au ceramic tiles kujua ipi ina uwezo mkubwa zaidi wa kuhimili mipasuko.

Architect Sebastian Moshi

+255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *