MALIGHAFI YA CHUMA

Sehemu kubwa ya ujenzi wa majengo yanayojengwa kwa mihimili ya chuma hufanyika na aina ya chuma inayoitwa “mild steel” au chuma laini. Hii ni aina ya chuma ambayo ni imara sana. Kwa mfano chuma ya aina hii yenye kipenyo cha wastani wa sentimita 25 mpaka 30 ina uwezo wa kunyanyua au kuning’iniza mzigo wa tani 20 bila kukunjika wala kuvunjika.

Mihimili ya chuma ina nguvu ya kuhimili uzito mkubwa

Sifa nyingine ya ujenzi wa jengo lilijengwa kwa kutumia chuma ya aina hii ni wepesi wa kujikunja bila kuvunjika(flexibility), inaweza kukunjika bila kuvunjika au kupata mipasuko, na hili huweza kusababishwa na upepo mkali au tetemeko la ardhi.

Hivyo mihimili hii ya chuma inapokutana na msukumo mkubwa au presha kubwa haiwezi kuvunjika ua kupasuka ghafla kama kioo badala yake inajikunja taratibu kutoka kwenye umbo lake la awali.

Mihimili ya chuma hata haivunjiki wala kupasuka bali inajikunja taratibu.

Kujikunja huku kunawapa fursa wakazi wa jengo husika kupata kwanza onyo la kuondoka kabla jengo halijaanguka na kuleta madhara. Kuanguka kwa mihimili ya chuma hakutokei ghafla na ni mara chache jengo kuanguka moja kwa moja kabla halijaokolewa. Mara nyingi jengo lililojengwa kwa mihimili ya chuma hufanya vizuri zaidi kwenye tetemeko la ardhi kuliko malighafi nyingine kama vile zege kwa sababu ya sifa hizi za kipekee

Changamoto kubwa ya malighafi ya chuma katika mihimili ni sifa yake ya kupoteza uimara wake kwa haraka jengo linapokumbwa na moto. Joto linapofika nyuzijoto 500 hizi chuma laini huweza kupoteza mpaka nusu ya uwezo wake. Na hiki ndicho kilichotokea katika majengo ya World Trade Centers katika jiji la New York, nchini Marekani yalipolipuliwa na magaidi wa Al-Aaeda wakiongozwa na Osama bin Laden mwaka 2001.

Mihimili ya chuma ina changamoto za kudhoofika haraka inapokutana na joto kali.

Hivyo chuma katika majengo yanapaswa kulindwa na kuepushwa na moto au joto kali ambapo hili hufanyika kwa kuyafunga na malighafi inayozuia moto au kupulizia dawa maalumu ya kuzuia moto.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *