JE, JENGO/NYUMBA YAKO INAPANDISHA UNYEVU UNAOHARIBU RANGI YA NYUMBA?

Kuna changamoto kubwa inayozikabili nyumba nyingi hasa zilizojengwa kwenye maeneo ambayo kina cha maji hakiko mbali sana chini ardhini. Ni tatizo ambalo limekuwa sugu na hupelekea kuharibu rangi ya nyumba kwa kuanzia chini kupanda juu ambapo hupelekea nyumba kupoteza ubora wake, kushuka thamani na hata kupoteza mvuto.

NYUMBA ILIYOATHIRIWA NA UNYEVU

Sababu kubwa ya changamoto hii ni ufundi wa mwanzo kutokuzingatia hatari hii na hivyo kutoweka karatasi pana la dpm chini kabla ya kumwaga zege(jamvi) la sakafu ya chini. Karatasi/zulia hili la plastiki la dpm(damp proof membrane) huwa ni maalumu kwa kuzuia unyevu kupanda na nyumba pamoja na namna yoyote ya umajimaji, unyevu na uharibifu mwingine wa kikemikali unaoweza kuleta madhara kwenye nyumba.

UNYEVU KUENDELEA KUPANDA KUHARIBU KUTA

SULUHISHO.

Kwa kesi ambayo nyumba ilishajengwa na madhara yameanza kuonekana suluhisho la changamoto hii ni kufanya ukarabati wa nyumba nzima kuziba yale maeneo yanayopandisha unyevu kwa kutumia vipande vya karatasi/zulia la plastiki ya dpm kuzunguka nyumba nzima. Hii inafanyika kwa kuchimba(drilling) ya ukuta kwa chini kwa vipande vidogo vidogo kwa uangalifu mkubwa kisha kuweka dpm. Katika kufanya drilling kunatakiwa uangalifu mkubwa kwa kuzingatia kufanya kwa vipande vidogo vidogo kuepuka kudhoofisha sehemu kubwa ya jengo kwa wakati mmoja. Kila baada ya kumaliza kipande kimoja unaweka dpm na juu yake wiremesh kisha kufanya plastering. Baada ya kumaliza nyumba nzima unarudia kupaka rangi upya maeneo yote yaliyoathirika kurudisha jengo katika ubora wake wa mwanzoni. Baada ya hapo utakuwa umemaliza changamoto hii.

KUFANYA DRILLING ILI KUWEKA VIPANDE VYA DPM

Kwa kesi ambayo jengo ndio linaanza kujengwa ni muhimu sana katika hatua za ufundi kuzingatia kuwekwa zulia la plastiki la dpm baada ya kumaliza kujenga kuta za msingi na kurudishia udongo hatua ya kabla ya kushughulika na sakafu ya chini ya jengo.

KUTANDAZA ZULIA LA DPM KATIKA HATUA ZA MWANZO ZA UJENZI

Ukarabati huu ni muhimu sana katika kuiweka nyumba/jengo kwenye ubora wakati wote.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *