UDONGO HATARI UTAKAOLETA NYUFA KWENYE NYUMBA YAKO.

Kuna watu wamekuwa wakishangaa nyumba zao kupata nyufa ambazo wakati mwingine huwa kubwa kiasi cha kudhoofisha nyumba na kuhitaji ukarabati upya bila kujua mahali hasa zilipotokea nyufa hizo.

Changamoto hii nimekutana nayo mara kadhaa ambapo wahusika wamekuwa wakipata hofu sana na wasijue hasa chanzo chake na nini cha kufanya.

Kuna aina za udongo laini na unaoteleza ukiloweshwa hasa mfinyanzi ambazo wakati wa mvua huloa na kulainika sana kisha likipiga jua kali hukauka na kujikunja sana ambapo udongo huu katika kujikunja sana hubana msingi wa nyumba na kuufinyanga kwa nguvu kiasi cha kuukata na kusababisha mipasuko na nyufa ambazo hupanda na nyumba kuelekea juu.

UDONGO MFINYANZI UNAPOKAUKA NA KUKAKAMAA

Ukubwa wa nyufa na uharibifu wa nyumba hutegemea na msukumo mkubwa wa udongo huu ambao huwa chini kwenye msingi wa nyumba. Hii ni kutokana na hatua za ujenzi wa msingi ambapo mafundi wengi aidha kwa kutokujua au kwa makusudi hurudishia udongo wote walioutoa baada ya kukamilisha ujenzi wa kuta za msingi hivyo kuja na madhara baada ya muda.

NYUFA KATIKA JENGO ZILIZOANZIA KWENYE MSINGI

SULUHISHO.

Kama eneo inapojengwa nyumba lina aina ya udongo usiofaa wakati wa kujenga msingi ndio wakati muhimu zaidi kuwa makini na kinachoendelea katika hatua hii ya ujenzi. Mjenzi anapaswa baada ya kuchimba msingi wa jengo asirudishie tena udongo usiofaa badala yake ununuliwe udongo mwingine au mchanga ndio urudishiwe kwenye msingi baada ya kumalizika kujengwa kwa kuta za msingi wa nyumba(foundation walls). Mchanga na aina nyingine za udongo ambao hautelezi wala haulainiki na kukauka ndio udongo sasa kurudishia kwenye msingi(backfilling) ili kuepuka madhara haya. Kwa nyumba ambayo tayari imeshaathiriwa na changamoto hiyo inaweza kufanya “underpinning” kujua tatizo na kisha kutafuta njia sahihi ya kulitibu kulingana na asili ya tatizo husika.

NYUFA HUENDELEA KUTANUKA KADIRI YA KUVIMBA NA KUKAKAMAA KWA UDONGO MFINYANZI

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *