NI MUHIMU KUHAKIKI VIPIMO VYA JENGO LAKO.

Wewe kama mmiliki na mtumiaji wa jengo baada ya kupata mtaalamu wa kukutengenezea ramani nzuri na sahihi kuna mambo unatakiwa kuwa nayo makini wakati mchakato wa kuandaa ramani na michoro unaanza na mojawapo ni kuhakikisha unaelewa kwa usahihi vipimo halisi vya jengo lako badala ya kumuachia mtaalamu ndio akuamulie. Kumuachia mtaalamu ndio akuamilie huwa wakati mwingine inapelekea majuto fulani hapo baadaye kwa sababu.

-Kwanza wewe ndiye mtumiaji wa jengo hivyo na sio yule mtaaamu wewe ndio unajua kwa usahihi unahitaji vyumba vya ukubwa gani kwa sababu kutoka kwenye uzoefu unajua wapi utataka kuongeza na wapi utataka kupunguza.

WEWE NDIYE MTUMIAJI WA JENGO NA NDIYE UNAYEFAHAMU UNAHITAJI UKUBWA GANI NA SIO MTAALAMU ANAYECHORA

-Unaweza kuelewa hasa ukubwa unaotaka kwanza kwa kulinganisha na unapoishi kwa sasa, kwanza uchukue vipimo vya unapoishi kwa sasa kisha ulinganishe na vipimo vilivyochorwa na kisha uone kama ndio ukubwa huo unaohitaji au utataka kuongeza au kupunguza. Hili ni rahisi kwa sababu tayari umejionea mwenyewe na unatoa kwenye uzoefu.

FAHAMU UKUBWA UNAOTAKA KWA KULINGANISHA NA ENEO UNALOISHI KWA SASA KISHA UTAONGEZA UA KUPUNGUZA KADIRI YA CHANGAMOTO NA MANUFAA UNAYOYAPATA PALE UNAPOISHI KWA SASA

-Njia nyingine nzuri ya unahitaji ukubwa gani ni kufahamu una mpango wa kuweka nini ndani na unataka kubakiwa na ukubwa gani baada ya hapo. Angalia ukubwa wa fenicha unazotaka kuweka kisha linganisha na ukubwa halisi unaoutaka na eneo la ziada ambalo ungependa kubaki nalo. Hii itakupa ukubwa sahihi unaohitaji.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *