MRADI WA UJENZI UPANGILIWE KABLA YA KUANZA
Kumekuwa kunajitokeza changamoto nyingi wakati mradi ukiwa unaendelea ambazo wakati mwingine huleta hasara ya fedha na muda zinazosababishwa na kutokuwa na mpangilio sahihi wa mtiririko wa namna mradi utatekelezwa. Hili linatakiwa kufanyika kwa timu nzima ya ujenzi kwa maana ya watu wa fani zote wanaohusika kukaa pamoja, kujadili na kila mtu atazungumzia upande wake kisha mwishoni watakubaliana kuhusu mpangilio sahihi wa kazi utakaoleta mtiririko usiojichanganya wenyewe.
Kutopangilia mradi wa ujenzi mwanzoni hupelekea kutojua nini kinapaswa kuwa kipaumbele na kikifuatiwa na nini na hilo limesababisha kufanyika makosa mbalimbali yanayokuja na hasara ya fedha, muda pamoja na ubora.
Kwa mfano utakuta watu wanaohusika na ujenzi “masonry work”, wameshakamilisha kumimina zege maeneo yote kabla mtaalamu anayehusika na umeme hajafunga mfumo wa mabomba ya umeme(conduit pipes systems) ambayo yanatakiwa kuwa yalishafungwa kabla zege za mifumo ya mihimili haijafungwa, na hilo linapelekea gharama kubwa ya kufunga tena au kutindua upya kitu ambacho kinaleta usumbufu na hata kupoteza ubora na ufanisi wa mfumo huo wa umeme.
Au unakuta watu wa ujenzi “masonry” wamekamilisha kazi ya “plasta” na watu wa kufanya “skimming” na kupiga rangi nao wamemaliza kazi yao lakini watu wa vyuma vya kuchomea “welding” bado hawajaanza kazi yao, jambo hili linapelekea kurudia rudia kazi mara mbali jambo linaloongeza gharama ya muda, fedha, ubora na uimara wa jengo.
Hivyo kazi yoyote inapaswa kupangiliwa vyema mwanzoni kabla ya kitu chochote kuanza jambo amablo litasaidia sana kazi kwenda vizuri, kwa usahihi na kwa viwango bora.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!