AINA ZA UKARABATI WA JENGO

UKARABATI WA JENGO

-Ukarabati unahusisha kazi katika jengo ambazo zinafanyika ili kuliweka jengo katika hali sahihi inayopelekea jengo kutimiza kusudi lake au kufanya kazi kwa usahihi kwa kadiri ililivyokusiwa.

UKARABATI UNAFANYIKA KULIWEKA JENGO KATIKA HALI SAHIHI

AINA ZA UKARABATI WA JENGO

(i)UKARABATI WA KILA MARA

Hii ni aina ya ukarabati unaoweza kufanya kila inapotokea changamoto katika jengo la huduma zake, inaweza kuwa ni umeme wa kurekebisha au bomba lililoziba au kupata hitilafu nyingine yoyote kuitatua, kufyeka nyasi au kukatia uzio wa miti, kumwagilia nyasi, kufagia na kusafisha mazingira n.k.,

UKARABATI UNAWEZA KUFANYIKA INAPOTOKEA CHANGAMOTO

(ii) UKARABATI WA KILA MWAKA

Hii ni aina ya ukarabati unaofanyika kila mwaka kuboresha jengo kwa kuchunguza maeneo ambayo ubora wake umefifia na kuyakarabati mpya kama vile rangi ya jengo, madirisha, uchakavu wa paa n.k., kuhakikisha kila wakati jengo linang’aa sana na kupendeza muda wote.

UKARABATI UNAWEZA KUWA UNAFANYIKA KILA BAADA YA KIPINDI FULANI KWA MFANO MWAKA MMOJA

(iii)UKARABATI MAALUM

Ukarabati maalum ni aina ya ukarabati wa jengo ambapo baadhi ya maeneo ya jengo yalIoharibika sana au kuwa katika hali mbali yanaondolewa kabisa na kuwekwa mengine. Hii inasaidia jengo kubaki kama jengo jipya wakati wote na uzuri wa jengo husika kutofifia.

UKARABATI MAALUM UNAHUSHISHA KUBADLISHA BAADHI YA “ELEMENTS” ZA JENGO

(iv)UKARABATI WA KUONGEZA NA KUBADILI BAADHI YA VITU KWENYE JENGO

Hii ni aina ya ukarabati ambapo kunatokea uhitaji wa kuongeza baadhi ya vyumba au vifaa na huduma ndani ya jengo ili kukidhi mahitaji mapya ya mtumiaji yaliyojitokeza. Hii aina ya ukarabati mara nyingi huhusisha hata kubadili samani za ndani ya jengo.

UKARABATI WAKATI MWINGINE UNATOKANA NA MAHITAJI MAPYA YA MTUMIAJI

(v) UKARABATI WA KUZUIA UHARIBIFU. Hii ni aina ya ukarabati wa jengo ambao huhusisha uchunguzi wa mara kwa mara wa jengo kujua kama kuna kazi zozote zinazopelekea uharifu wa jengo hilo utakaoonekana baada ya muda ambao aidha unasababishwa na watu, wadudu, hali ya hewa au zoezi lingine lolote ambapo baada ya uchunguzi huu hatua sahihi za kuzuia uharibifu huu hufanyika

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *