UKARABATI WA MIFUMO YA ZEGE KWENYE JENGO(MAITENANCE OF CONCRETE STRUCTURES).

Malighafi ya zege ni malighafi inayodumu kwa miaka mingi sana hasa kwenye zama hizi ambazo teknolojia ya ujenzi imefika mbali sana, kama ikijengwa kwa kuzingatia ubora na uimara inaweza kudumu kwa karne kadhaa.

Kuchelewa kufanya ukarabati wa mifumo ya zege inayoharibika hupelekea gharama za marekebisho kupanda zaidi kila siku hivyo kuwa gharama kubwa kadiri muda unayoendelea kwenda mbele.

Ukarabati wa mifumo ya zege unahusisha kuzuia uharibifu wa mifumo ya zege unaotokana na hali ya hewa au mazingira ya mifumo hii ya zege kama vile maeneo yenye unyevu mwingi, maeneo yenye maji kama vile kwenye madaraja, baharini ay ziwani au hata maji kutoka chini ardhini.

MIFUMO YA ZEGE YA KISASA IKIJENGWA KWA KUZINGATIA UBORA NA UIMARA INAWEZA KUDUMU KWA KARNE KADHAA

Ukarabati huu unafanyika kwa kuhakikisha zege husika inakuwa na vizuizi vinavyozuia maji au unyevu kupenya ndani na kuozesha zege yenyewe na pia kwenda kuozesha malighafi nyingine ndani ya zege kama vile chuma amabyo hupigwa na kutu na kisha kumomonyoka.

KUCHELEWA KUFANYA UKARABATI WA MIFUMO YA ZEGE KWENYE MIHIMILI YA JENGO HUPELEKEA GHARAMA ZA KUFANYA HIVYO KUWA KUBWA SANA

Ukarabati wa mifumo ya zege unaweza kufanyika pia kwa kuziba maeneo ambayo unyevu au maji yanaingilia kwa kutumia kemikali maalum za mafuta au rangi ambayo hupakwa kwenye tabaka la mwanzoni la mifumo hii ya zege.

KUZUIA MAJI KUINGIA NDANI YA ZEGE KWA KUTUMIA KEMIKALI AU TABAKA ZA PLASTIKI KUTASAIDIA KUZUIA CHUMA ILIYOPO NDANI YAKE KUTOPATA KUTU NA KUMOMONYOKA

Hata hivyo njia na mbinu zinazotumika kwenye ukarabati wa mifumo hii ya majengo unategemea na ukubwa wa tatizo na changamoto husika na kama tatizo limekuwa kubwa sana pengine litahitaji kufanya marekebisho makubwa sana au kuondoa kabisa eneo liliharibika na kulijenga upya ila kwa kuzingatia kwamba tayari hayo ni mazingira yatakayopelekea zege hiyo kuharibika na kumonyonyoka tena baada ya muda hivyo kuhakikisha njia zinazotumika tena ni njia zitakazotibu tatizo.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *