UKARABATI WA MIFUMO YA CHUMA KWENYE JENGO(MAINTENANCE OF STEEL STRUCTURES).

Malighafi za chuma katika ujenzi huweza kuharibika kwa kupigwa kutu na kumomonyoka kiasi cha kuanza kudhoofisha uimara wa jengo ambapo kama utaendelea kuachwa utaleta hatari ya jengo kuvunjika na kuanguka.

Kufanya ukarabati wa mifumo ya chuma kwenye jengo ni kazi inayohitaji umakini mkubwa na ambayo inahusisha hatua nyingi muhimu kuweza kuifanikisha.

UKARABATI WA MIFUMO YA CHUMA UNAHITAJI UMAKINI MKUBWA

Kuna njia mbili za kukarabati mifumo ya chuma kwenye jengo ambayo imeharibika au kuanza kuoza ambazo ni moja ni kuimarisha chuma yenyewe kwa kuiongezea na kuichomea(welding) vizuri kisha kuipaka rangi na nyingine ni kwa kuiondoa kabisa na kuweka nyingine upya na kisha kupaka rangi ya kuzuia uharibifu mwingine wowote.

UKARABATI WA MIFUMO YA CHUMA WAKATI MWINGINE HUHITAJI KUZIONDOA KABISA NA KUWEKA MIFUMO MINGINE MIPYA

Chuma au nondo wakati mwingine huwa ziko ndani ya zege, hivyo inahitaji mtu kutindua zege ili kuweza kufanya ukarabati huo ambapo baada ya kumaliza aidha kuimarisha kwa kuiongezea na kuichomea au kuibadilisha kabisa basi unarudishia zege hiyo lakini pamoja na kuweka vizuizi(sealants) vya kuzuia uharibifu mwingine kama huo kutokea.

WAKATI MWINGINE UTAHITAJI KUFANYA UKARABATI WA CHUMA ILIYOKO NDANI YA ZEGE

Changamoto kubwa ya chuma mara nyingi huwa ni kupigwa na kutu ambayo huendelea kuimaliza taratibu hivyo ni muhimu kuhakikisha unaweka vizuizi vya ukuzia uwezekano wa chuma hiyo kupata kutu aidha baada ya kuibadilisha au kuweka nyingine.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *