KUCHORA NA KUJENGA(DESIGN AND BUILD)

Kuchora na kujenga/design and build ni njia ya kutekeleza mradi wa ujenzi ambapo mradi mzima kuanzia kuchora mpaka kukamilisha ujenzi wa mradi mzima unasimamiwa na mtu mmoja au kampuni moja inayosimama kama kiongozi wa timu nzima ya wataalamu itakayohusika kwenye mradi huo badala ya kutoa zabuni kwa kila mtaalamu anayehusika kila mmoja kufanya peke yake na kivyake bila kuwa kama timu.

MRADI UNAFANYWA KWA USHIRIKIANO NA TIMU YOTE YA WATAALAMU WANAOHUSIKA KWENYE MRADI MZIMA CHINI YA USIMAMIZI MMOJA

Katika njia hii ya kuchora na kujenga/design and build method, mtu mmoja au kampuni moja inayoingia mkataba wa mradi huu ndio inayotafuta na kuajiri au kuingia mkataba na wataalamu wengine wote watakaohusika katika kufanikisha mradi husika kwa viwango vilivyoamuliwa.

KAMPUNI MOJA INAAJIRI NA KUINGIA MKATABA NA KAMPUNI NYINGINE ZOTE ZITAKAZOHUSIKA KWENYE MRADI HUSIKA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *