FAIDA ZA KUTEKELEZA MRADI KWA NJIA YA KUCHORA NA KUJENGA/DESIGN AND BUILD

-Wataalamu wote kufanya kazi kama timu: mara nyingi kwenye miradi ya ujenzi huwa kunatokea mivutano na kutokuelewana baina ya upande wa mkandarasi(contractor) na upande wa washauri wa kitaalamu(consultants) ambayo huathiri mradi kwa namna moja au nyingine lakini kwenye njia hii ya kuchora na kujenga wataalamu wote wanafanya kazi pamoja hivyo kuepusha mivutano.

KWENYE NJIA YA KUCHORA NA KUJENGA WATAALAMU WOTE WANAKUWA NI TIMU MOJA

-Eneo moja la uwajibikaji: Kwa kawaida mradi wowote wa ujenzi huwa na vitengo vya kitaalamu visivyopungua vitano na wakati mwingine vinaenda mpaka kumi au zaidi japo hata hivyo vitengo vikuu huwa ni viwili ambavyo ni timu ya washauri wa kitaalamu(consultants team) na upande wa timu wakandarasi kuanzia mkandarasi mkuu(main contractor) mpaka wakandarasi wadogo(subcontractors), ambapo yanapofanyika makosa huwa kuna upande unaobeba lawama na hivyo mteja mwenye mradi hujikuta akilazimika kujihusisha na wataalamu tofauti tofauti katika kukabiliana na changamoto za mradi husika na wakati mwingine hutokea mivutano baina ya wataalamu hawa, lakini kwenye njia hii ya kuchora na kujenga mteja hujihusisha na upande mmoja peke yake au mtu mmoja peke yake aliyeingia mkataba wa kusimamia mradi wote mpaka kukamilika.

TIMU NZIMA ITAWAJIBIKA KWA CHOCHOTE KITAKACHOTOKEA KWENYE MRADI

-Mijadala ya wazi: Kwenye miradi ya ujenzi licha ya kila upande kuleta taarifa na nyaraka zote zinazoeleza kila kitu kinachoenda kufanyika kwenye ujenzi lakini kuna vitu vingi ambavyo hujitokeza na kuleta mivutano wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi, kwa sababu kila upande huw ana sababu zake, uzoefu, maslahi binafsi pamoja na utamaduni wake wa namna ya kufanya kazi lakini kwenye njia hii ya kuchora na kujenga inayoongozwa na mtu mmoja kila kitu hujadiliwa kwa uwazi na hivyo kuepusha mivutano na kupishana sana kwenye changamoto zinazojitokeza wakati wa ujenzi.

KWENYE NJIA YA KUCHORA NA KUJENGA KILA KITU HUJADILIWA KWA UWAZI NA KUEPUSHA MIVUTANO NA MRADI KUMALIZIKA KWA MUDA ULIOPANGWA

-Mradi kukamilika kwa haraka: Njia hii ya kujenga na kuchora husaidia mradi kukamilika kwa muda uliopangwa au hata mapema zaidi kwa sababu ya uharaka wa kila maamuzi yanayopaswa kufanyika kutokana na timu nzima kufanya kazi kwa pamoja na kuwa kwenye maelewano kuanzia mwanzo kabisa wakati wa kuandaa michoro ya ramani.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *