UBORA WA RAMANI YA JENGO.

Nini maana ya ubora wa ramani ya jengo?

Ramani ya jengo yenye ubora ni ramani ambayo imefanyika kwa usahihi unaohutajika kwa maana ya kwamba ni ramani inayozingatia viwango sahihi kwenye kila eneo kuanzia vipimo sahihi, uelekeo sahihi, mpangilio sahihi wa kimatumizi, mpangilio sahihi wa vitu vinavyoamua uzuri wa muonekano wa jengo husika, mapendekezo sahihi ya malighafi ya ujenzi pamoja na kuzingatia viwango vilivyowekwa na mamlaka zinazohusika kusimamia ujenzi.

RAMANI YENYE UBORA NI ILE ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANGO SAHIHI

Matokeo ya ubora wa ramani ya jengo mara nyingi huja kuonekana baadaye wakati jengo linapokuja kuanza kutumika ambapo kama kuna mambo yalifanyika bila kufuata utaratibu sahihi au kuzingatia viwango sahihi kwenye kila eneo la jengo ndipo madhara yake huanza kuwa wazi. Mengine huweza kurekebishika na mengine hushindikana kurekebisha baadaye.

MATOKEO YA RAMANI ILIYOKOSA UBORA HUJA KUONEKANA BAADA YA JENGO KUANZA KUTUMIKA

Ubora wa ramani ya jengo siku zote hutokana na ubora wa mtaalamu anayefanya kazi husika sambamba na uzoefu alionao kwa maana ya uwingi wa kazi na changamoto alizopitia katika kufanya kazi zake na matokeo ambayo ameshakutana nayo. Uwezo na uzoefu vinakwenda pamoja, hivyo kama unahitaji kupata ramani ya jengo yenye ubora ambayo haitakuja kukuletea usumbufu baadaye unahitaji kufanya kazi na mtu mwenye uwezo na uzoefu katika fani ya majengo ambaye ameshakabiliana na changamoto nyingi za kuhusu majengo na ameshakutana na matokeo ya kazi zake nyingi alizofanya.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *