MUDA NI FEDHA, KASI NI THAMANI.

Kadiri kitu kinavyoweza kufanyika kwa haraka zaidi lakini kwa ubora ule ule gharama ya kukikamilisha huwa inakuwa kubwa zaidi kuliko kinapofanyika kwa kutumia muda mrefu zaidi. Mfano mzuri ni kwenye usafiri, kwamba pamoja na mambo mengine kama vile usalama na mazingira bora ya ndani ya chombo cha usafiri, lakini usafiri unaowahi zaidi huwa na gharama kubwa zaidi ukilinganisha na usafiri unaochelewa na thamani ya ziada hapo ni muda unaookolewa.

KASI ZAIDI KWA VIWANGO VILE VILE VYA UBORA NI GHARAMA ZAIDI

Tukija kwenye ujenzi pia mambo hayako tofauti sana, pale ambapo ubora wa kazi na rasilimali ziko sawa mkandarasi anayeweza kukamilisha mradi kwa muda mchache zaidi kwanza ni yule mwenye uzoefu zaidi na uwezo zaidi, lakini pia ndiye anayechukuliwa ni wa thamani zaidi kwani anakuwa ameokoa rasilimali muda ambayo inaleta manufaa mengine kama vile jengo kuanza kutumika mapema zaidi na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa kwa haraka zaidi.

MKANDARASI ANAYEKAMILISHA MRADI WA UJENZI KWA HARAKA ZAIDI KWA VIWANGO SAHIHI LAKINI KWA RASILIMALI FEDHA SAWA NI YULE MWENYE UZOEFU NA UWEZO MKUBWA NDIO MAANA ANAONGEZA THAMANI HII YA MUDA.

Ikiwa unahitaji kufanya kazi yako kwa haraka zaidi lakini kwa ubora na kwa viwango vya juu lakini kwa gharama za kawaida zisizolazimu kuongezeka kwa sababu ya kasi ambayo ni thamani ya ziada unaweza kuwasiliana nasi tukakupatia watalaamu wenye ubobeza mkubwa katika kuokoa muda lakini huku wakizingatia viwango vya ubora wa hali ya juu.

WAKO WATAALAMU WA KUKUKAMILISHIA MRADI KWA HARAKA ZAIDI NA KWA VIWANGO VYA JUU LAKINI KWA GHARAMA ZA KAWAIDA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *