UNACHOHITAJI KUTOKA KWA MTAALAMU WA USANIFU MAJENGO(ARCHITECT) KWA AJILI YA KUANZA MRADI WA UJENZI.

Kama nilivyotangulia kusema katika makala zilizopita, usijaribu kujenga nyumba kabla ya kuonana na mtaalamu wa usanifu majengo(Architect) akupe mwongozo mzima wa kitaalamu sambamba na vigezo na masharti vilivyowekwa na mamlaka husika vinapaswa kufikiwa ili kupata kibali cha kuendelea na ujenzi, ukiendelea bila ushauri wa kitaalamu kuna nafasi kubwa sana kwamba unatafuta majuto mbeleni.

KUEPUKA KUINGIA KWENYE MIVUTANO NA MAMLAKA ZA UJENZI HAKIKISHA UNAPATA USHAURI WA KITAALAMU KABLA YA MRADI KUANZA

Kuweza kupatiwa kibali cha ujenzi na kuanza ujenzi wa jengo lako mtaalamu wa usanifu majengo atakupatia nyaraka zifuatazo.

-Seti saba za michoro ya ramani za ujenzi kama tulivyozifafanua kwenye makala iliyopita hapo juu zikiwa katika nakala za mafaili angalau matatu kadiri ya halmashauri husika itakavyokuwa inahitaji na wewe kupata nakala yako.

KILA HALMASHAURI YA MANISPAA AU MJI HUWA NA SHERIA ZAKE, TARATIBU ZAKE NA MASHARTI TOFAUTI NA HALMASHAURI ZA MANISPAA AU MIJI MINGINE

-Michoro hii inapaswa kuwa imezingatia taratibu zote zinazohitajika kitaalamu sambamba na viwango vilivyowekwa na halmashauri ya manisapaa husika juu ya mazingatio ya viwango vya matumizi ya ardhi ya eneo husika.

LAZIMA MICHORO IZINGATIE VIWANGO VYA MATUMIZI YA ARDHI VILIVYOWEKWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA AU MJI HUSIKA

-Michoro hii inapaswa kuwa imepigwa mihuri ya kampuni na kusainiwa na mtaalamu wa usanifu majengo aliyesajiliwa(Registered Architect) na bodi ya usanifu majengo na ukadiriaji majenzi(AQRB) anayetambulika kisheria kwa wakati husika.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *