KUEPUSHA KUHARIBU KAZI, MPE MTAALAMU UHURU WA KUTOSHA

Mara nyingi kama wewe ni mteja mtaalamu wa kufanya jengo huwa anakusikiliza unataka nini na kufanya unachotaka kwa sababu lengo lake ni kukuridhisha wewe na kufanya unachotaka kwa sababu wewe ndiye unayelipa pesa na mwisho wa siku wewe ndiye mmiliki wa jengo husika.

  • Changamoto huwa inatokea pale mteja ndio anakuwa mpangaji na mwamuzi wa kila kitu, kila anachotamani anataka kiwepo na wakati mwingine ndiye anaamua kiwekwe wapi licha ya kwamba hana utaalamu wala uzoefu wa kazi. Kinachotokea ni kwamba mtaalamu anaweza kuona sio sawa na kujaribu kuhoji lakini kwa kuwa mteja ametaka na anaamini vile anavyotaka ndio sawa mtaaalamu huweza kujikuta anafuata kila takwa na mteja na mwisho kazi kuharibika.
  • Kwa uzoefu wangu wa miradi mingi niliyokutana nayo, kazi za namna hii nyingi mwishoni huishia kutokea nzuri, sio tu kwa upande wa mipangilio ya kimatumizi bali hata ule uzuri wa kimwonekano mara nyingi huweza kupotea. Hii ni kutokana na kwamba mteja anakuwa hana utaalamu mkubwa wala uzoefu wa vitu vingi vinavyoathiri kazi husika, hivyo anaamua bila kuzingatia kanuni wala uzoefu wa kazi za nyuma hivyo anachoamua kinakuwa kina makosa mengi ya kiufundi ambayo yeye mteja sio rahisi kuyaona moja kwa moja na hivyo kusababisha kazi kutokuwa nzuri.
  • Hivyo jambo la msingi na la kuzingatia ni kwamba mteja anatakiwa kujua kila anachotaka na kueleza vyote anavyotaka kwa mtaalamu kisha kumwachia mtaalamu afanye kazi yake kitaalamu na kwa weledi mkubwa. Kisha baada ya kukamilisha waweke tena kikao na mteja na kujadili kila kitu kuangalia kilichowezekana na kilichoshindikana, na ambapo sasa mteja atakuja na mapendekezo mengine tena watakayoyafikiria upya na kufikia maamuzi lakini huku mtaalamu akipewa nafasi zaidi ya kutoa maoni sahihi bila kulazimisha sana kumfurahisha mteja kwa mbadala ambao utakuwa na changamoto sana.
  • Kwa kufanya hivi bila kuongozwa na hisia wala kulazimisha sana mambo mwisho kazi itapunguza makosa mengi yanayotokana na mteja kukosa uelewa mpana wa kitaalamu hivyo kazi kuwa na ubora wa hali juu kadiri inavyowezekana.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *