HATA KAMA KIWANJA CHAKO HAKIJAPIMWA NA KIKO KIJIJINI, SHIRIKISHA MTAALAMU.

Mradi wowote wa ujenzi unahusisha gharama kubwa sana za ujenzi hata kama unajengwa eneo la kijijini kiasi gani, na sio uamuzi wa busara hata kidogo kwenda kuweka pesa nyingi sehemu iliyokosa umakini na utaalamu. Mtaalamu wa ujenzi siku zote huongeza thamani ya mradi husika kwa kiasi kikubwa sana, kwa hiyo ni hasara kubwa unaingia unapoamua kutoshirikisha utaalamu kwa kigezo kwamba ni mradi unaojengwa eneo ambalo halina ulazima wa kushirikisha mtaalamu wa ujenzi.

THAMANI YA MRADI WOWOTE INAONGEZWA NA UTAALAMU ULIOHUSISHWA

Hivyo bila kujali mradi wako unajengwa wapi, pale unapoanza kufikiria kuhusu kuanza mradi husika hakikisha hatua ya kwanza ni kukaa chini na mtaalamu wa ujenzi kujadili mradi huo. Ke akufanya hivyo utakuja kufurahia sana matokeo ya mwisho ambayo kwa vyovyote vile unatamani yawe matokeo bora na yenye thamani kubwa.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *