BILA KUFUATILIWA NA MSIMAMIZI MTAALAMU, KAZI YOYOTE YA UJENZI ITAHARIBIKA.

Katika kitu ambacho hutokea karibu mara zote katika mradi wa ujenzi ni pamoja na mabadiliko ya jengo wakati wa kujenga ambayo yanaleta utofauti kidogo na michoro ya mwanzo iliyokusudiwa. Mabadiliko hutokea mara zote na siku zote, wakati mwingine yakisababishwa na changamoto zilizojitokeza wakati wa ujenzi na wakati mwingine yakisababishwa na maamuzi ya mteja mwenyewe baada ya kuona haja ya kufanya hivyo.

MABADILIKO MADOGO MADOGO HUTOKEA MARA ZOTE

Mabadiliko yoyote yanayofanyika wakati wa ujenzi ni lazima yanakuwa na madhara kwa sababu mpangilio uliowekwa mwanzoni unavurugwa, na katika vitu ambavyo huwa vinafanyika kwa mpangilio na utaratibu makini sana ni pamoja na michoro ya jengo hivyo chochote kitakachofanyika siku zote huja na madhara yake chanya au hasi.

MABADILIKO YOYOTE HUATHIRI MPANGILIO WA JENGO KIMUONEKANO NA KIMATUMIZI

Ili mabadiliko yanayofanyika yawe na madhara chanya na yalete matokeo yenye manufaa ni lazima yafanywe na mtaalamu ambaye atazingatia athari zote zitakazojitokeza kutokana na mabadiliko hayo, iwe ni athari za nje kwa maana ya muonekano wa jengo au athari za ndani kwa maana ya kuvuruga mpangilio wa kimatumizi ndani ya jengo kama vile faragha, nafasi n.k.

ILI MABADILIKO YASIWE NA MADHARA HASI NI LAZIMA YAFANYWE NA MTAALAMU WA UJENZI AMBAYE ATAZINGATIA ATHARI ZA AINA ZOTE ZINAZOLETWA NA MABADILIKO HAYO NA KUZITATUA

Mabadiliko yanapofanyika kiholole huja na madhara hasi kwani hayazingatii kabisa athari mbalimbali za jengo ambazo mtaalamu ndiye anaweza kuziona kutokea kwenye kila pembe ya kimtazamo ya jengo husika ambapo mtu wa kawaida sio rahisi kuona mpaka atakapoanza kulitumia jengo hilo wakati mradi umeshamalizika. Ndio maana tunasema bila mradi wa ujenzi kufuatiliwa kwa karibu na mtaalamu msimamizi kazi hiyo ina nafasi kubwa kabisa ya kuharibika au madhara yake kuja kuonekana wakati jengo litakapoanza kutumika.

KAZI YOYOTE YA UJENZI ILI ISIHARIBIKE NI LAZIMA IFUATILIWE KWA KARIBU NA MTAALAMU MBOBEZI

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *