VIKAO VYA KWENYE ENEO LA UJENZI(SITE MEETINGS)

Kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na mamlaka husika, kila mradi wa ujenzi hutakiwa kuwa na vikao vya mara kwa mara kwa ajili ya kujadili maendeleo ya mradi kuanzia masuala ya kiufundi ya kazi, fedha, ratiba ya kazi juu ya muda uliopangwa, mabadiliko, maamuzi mbadala pamoja na changamoto nyingine zinazoweza kuwa zinaukabili mradi husika.

CHANGAMOTO KUBWA NA ZENYE MADHARA MAKUBWA HUWEZA KUTATULIWA KWA USAHIHI PALE PANDE ZOTE TATU ZINAFANYA KIKAO

Vikao hivi vinavyojulikana kama “site meetings” ambavyo vinahudhuriwa na mtaalamu mshauri mkuu wa mradi pamoja na timu yake, mkandarasi pamoja na timu yake, pamoja na mteja ai mwakailishi wake ndivyo husaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mradi wa ujenzi kwa usahihi zaidi na kwa kuzingatia pande zote za tatizo husika, hivyo ni vikao muhimu sana.

Hivyo kwa mradi ambao haujafuata taratibu za kisheria ni muhimu kuendesha kwa namna hii ya vikao, jambao ambalo litasaidia sana kupata matokeo bora kabisa mwishoni. Ni jambo litakalohitaji kupangilia ratiba hizi za vikao vya ujenzi mwanzoni, labda mara moja kwa mwezi au mapema zaidi kadiri ya kasi ya mradi husika ili kuepuka kwenda mbali sana bila kutatua changamoto zinazojitokeza kabla ya tatizo kuwa kubwa na kupelekea utatuzi wake kuwa ni changamoto sana au kushindikana kabisa.

MRADI AMBAO HAUJAFUATA TARATIBU ZA KISHERIA NI VYEMA KUUENDESHA KWA MFUMO HUU WA VIKAO ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KWA USAHIHI NA KUHAKIKISHA MATOKEO BORA YA MRADI HUSIKA

Vikao husika vinatakiwa viwakilishwe na pande tatu, upande wa mtaalamu mshauri(consultancy), mkandarasi(contractor) na mteja(client). Lakini hata ikiwa radi hauna upande wa mtaalamu mshauri(consultancy) basi angalia kikao kifanyike na upande wa mkandarasi na mteja, vikao hivi ni muhimu na vina msaada mkubwa sana kwenye kuhakikisha matokeo ya mwisho yanakuwa yenye ubora sana.

Archutect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *