DAFTARI LA MAELEKEZO(INSTRUCTION BOOK)

Katika eneo la ujenzi(site) mambo huwa ni mengi sana na maamuzi yanayopelekea mabadiliko mbalimbali hufanyika mara kwa mara sana kiasi kwamba kama maamuzi hayo hayajawekwa kwenye maandishi ni rahisi baadhi ya mambo kusahaulika hivyo kutoingizwa kwenye utekelezaji kwa usahihi kama ilivyoamuliwa na matokeo yanayokusudiwa kushindwa kufikiwa.

BAADHI YA MAMBO NI RAHISI KUSAHAULIKA YASIPOWEKWA KWENYE KITABU CHA MAELEKEZO

Hivyo ni muhimu sana kuwepo kwa daftari la maelekezo au “instruction book” ambalo kazi yake ni kuandikwa kila kinachoamuliwa na tarehe ambayo maamuzi hayo yamefanyika na hivyo kabla ya kufanya maamuzi yoyote wale wanaofanya maamuzi wanapaswa kufahamu maamuzi yote yaliyofanyika siku zilizopita kupitia “instruction book” ili kujua mwelekeo wa mambo ulivyo na hivyo kufanya maamuzi sahihi na yanayofuata mtiririko wa mwenendo wa mradi.

DAFTARI LA MAELEKEZO LINAONYESHA MTIRIRIKO WA MAMBO ULIVYO HIVYO KUFANYA MAAMUZI YANAYOFUATA MTIRIRIKO SAHIHI

Kitabu hiki kitasaidia pia kuweka rekodi kwa usahihi juu ya mwenendo wa mambo na kusaidia kufahamu changamoto zote za mradi husika na namna zilivyotatuliwa na hivyo uzoefu huu kusaidia sana kupunguza makosana changamoto mbalimbali kwenye mradi mwingine wa aina hiyo.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *