HADHI YA NYUMBA ZA KUPANGA KIBIASHARA – KWENYE MIJI MIKUBWA TANZANIA

Nyumba nyingi za kupanga katika miji mikubwa ya Tanzania kwa ujumla na hasa Dar es Salaam zina changamoto nyingi sana hasa kwa upande wa hadhi ya nyumba zenyewe. Licha ya kwamba zinaweka viwango mbalimbali vya kodi lakini ni chache sana ambazo mteja anapata thamani sahihi ya ile pesa anayolipa, huku sababu kuu ikiwa ni kutozingatia kanuni za kitaalamu za kufanya “designs” sahihi za nyumba hizo pamoja na ujenzi wenyewe.

NYUMBA ZA KUPANGA ZILIZOKOSA UBORA NYINGI NI ZILE ZISIZOZINGATIA KANUNI ZA KITAALAMU

Kwa kutokuzingatia kanuni sahihi za kitaalamu nyumba nyingi za kupanga tunasema hazina hadhi ya kutosha kwa sababu, hazina mpangilio sahihi ndani ya nyumba na hivyo kuleta usumbufu kwa mtumiaji, hazina faragha ya kutosha, hazijafanyika kwa namna ya kusaidia kupatikana kwa mwanga wa asili na hewa ya asili ndani ya nyumba kwa viwango sahihi, mazingira yake ya nje hayajatengenezwa kwa namna inayoweza kumvutia mpangaji kwa usahihi kama parking sahihi, bustani n.k., ukubwa wa vyumba hauko katika viwango sahihi, hali mbaya ya majengo husika kwa kukosa ukarabati wa mara kwa mara unaohitajika n.k.,

KUNA VIGEZO KADHAA VINAVYOIFANYA NYUMBA YA KUPANGA KUPENDWA NA WATEJA SAHIHI NA BORA WASIO NA USUMBUFU

Bado ziko nyumba chache sana za kupanga ambazo ziko katika viwango na hadhi sahihi inayokidhi matakwa ya mtumiaji katika nyanja zote muhimu, na hizi ni zile ambazo zimeshirikisha huduma za kitaalamu kuanzia mwanzoni kabisa kabla ya ujenzi kuanza mpaka kukamilika kwa mradi mzima. Nyumba hizi zimekuwa zikiwapa wateja huduma bora sana za kuridhisha kiasi kwamba wateja wako tayari kulipia nyumba hizi gharama zaidi kutokana na huduma bora wanayoipata, na huwa zinapendwa na wateja bora wasio na usumbufu ukilinganisha na nyingine nyingi ambazo zinakosa vitu muhimu vya kumridhisha mteja kwa sababu tu ya kufanya kosa la kutohusisha utaalamu sahihi kabla ya kuanza mradi wenyewe.

WATEJA SAHIHI HAWANA USUMBUFU NA HUVUTIWA NA NYUMBA ISIYO NA USUMBUFU KWAO

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *