MAMBO YA KUZINGATIA IKIWA UNATAKA KUJENGA NYUMBA YENYE “BASEMENT FLOOR” KATIKA ENEO LENYE MWINUKO/MTEREMKO MKALI.

Jambo la kwanza na muhimu la kuzingatia ikiwa unataka kujenga nyumba yenye ghorofa inayoanzia chini ardhini maarufu kama “basement floor” katika eneo lenye mteremko mkali ni kina chake au ukali wa mteremko wenyewe. Wapo watu ambao wakishaona eneo lake lina mwinuko kidogo tu anataka kuweka ghorofa inayoanzia chini ardhini, lakini ukweli ni kwamba sio kila eneo linafaa kuweka ghorofa ya chini ardhini. Ni lazima kuwe na mteremko wenye kina cha kutosha kuweka “basement floor” bila kulazimisha sana na kupelekea matokeo yasiyoridhisha.

KUWE NA MTEREMKO WENYE KINA CHA KUTOSHA

Jambo lingine muhimu la kuzingatia ni ukali wa mteremko wenyewe(kina) ambapo kama mteremko ni mkali kupita kiasi ni muhimu kuzingatia kwamba kutahitajika kuchonga mpaka barabara inayoingia katika kiwanja hicho na hata bustani ya mbele ili kutengeneza vizuri na kwa usahihi eneo ambalo nyumba na mandhari yake ya nje vinakaa.

IKIWA ENEO LINA MTEREMKO MKALI SANA, ENEO ZIMA LINATAKIWA KUCHONGWA KWA USAHIHI

Jambo la tatu la kuzingatia sana ni mpangilio wa vyumba kwenye “basement floor”, kwa sababu ni muhimu kukumbuka kwamba ghorofa ya ardhini “basement floor” ina upande ambao ukuta wake umejishika na ardhi na hivyo hauwezi kupitisha hewa wala mwanga ndani ya jengo na hivyo utategemea kutumia kuta nyingine kupata vitu hivi, kwa hiyo upangiliaji wa vyumba unapaswa kuzingatia kikwazo hiki kujua namna sahihi kupangilia vyumba hivi huku mahitaji yote muhimu ndani ya chumba yanapatikana licha ya kuwepo kwa changamoto hii.

KUNAHITAJIKI UMAKINI MKUBWA KWENYE MPANGILIO SAHIHI WA VYUMBA UTAKAOSAIDIA UPATIKANANAJI WA HEWA NA MWANGA WA KUTOSHA KWENYE “BASEMENT FLOOR”

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *