MAPATANO YA BEI YA RAMANI NA KUJENGA YAWE NA MSINGI

Imekuwa ni changamoto sana kwa watu kupata uhakika kama gharama wanazolipa na kulipwa kwa huduma za ujenzi wanazotoa ni kiwango sahihi ama ni kubwa sana au ndogo sana. Hili wakati mwingine limekuwa likipelekea kukosekana kuridhika kwa pande hizo mbili na kwa kiasi fulani kuathiri ubora wa kazi pia. Jambo hili limekuwa likichangiwa na kukosekana na msingi wa bei hizi, kwamba nini kinapelekea bei iwe hiyo inayotajwa badala yake watu wanatajiana tu bila kuwa na msingi wa bei yenyewe.

KUKOSEKANA KWA MSINGI WA BEI KUNASABABISHA SINTOFAHAMU KWA PANDE ZOTE MBILI

Kwenye makala za nyuma niliwahi kuzungumza kwamba bei ya ramani inapaswa kuwa asilimia fulani ya bei ya gharama za mradi mzima wa ujenzi na nikapendekeza kwamba makadirio ya chini kabisa ni angalau asilimia 1% ya gharama za kujenga mradi wote wa ujenzi na kutokea hapo ndipo mnaweza kupatana mkianzia kwenye msingi huo. Mara nyingi kwa miradi mikubwa na inayohitaji umakini wa hali ya juu kwa michoro ya ramani peke yake bei hufika mpaka asilimia 3% ya gharama za mradi mzima, hivyo navyosema angalau asilimia 1% namaanisha kwa miradi ya kawaida ambayo haihitaji umakini mkubwa wala haikamati sana umakini wa mamlaka husika.

KWA MIRADI MIKUBWA GHARAMA ZA MICHORO ZINAFIKA MPAKA ASILIMIA 3% YA GHARAMA ZA MRADI MZIMA

Kwa upande wa gharama za ufundi wa kujenga pia bei ya ufundi inapaswa kuwa na msingi fulani ambao utawezesha mapatano yafikiwe bila malalamiko. Kwa wastani kwa makadirio ya chini sana bei ya ufundi wa kujenga majengo yasiyohitaji umakini mkubwa sana pamoja na majengo mengi ya watu wa kawaida mitaani gharama za ufundi kwa maana ya mkataba wa mkandarasi hufikia asilimia 30% ya gharama za vifaa. Hivyo asilimia 30% ndio inaweza kuwa msingi wa kuanzia katika mapatano ya bei za ufundi wa mradi mzima.

KWA MIRADI MIKUBWA GHARAMA ZA UFUNDI ZINAFIKIA ASILIMIA 35% MPAKA 40% ZA MRADI

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *